Madhara kuhusu mtazamo wa jamii kwa watu wasio na wenza 'Waseja'

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Kumuuliza mtu kwa nini "hana mwenza" na kumfariji kwamba "atapata mtu hivi karibuni" kunaweza kuonekana kama njia ya kufikirika na njia nzuri kujua jinsi marafiki zao wasio na wapenzi wanaendeleaje. Lakini misemo hii rahisi ni sehemu ya "aibu kwa wasio na wenza" na labda huleta madhara zaidi kuliko mema.

Hapa kuna baadhi ya hukumu dhidi ya waseja kwamba inaweza kuwa; labda lazima watakuwa na huzuni na wapweke kwa sababu hawana mwenza, wanatafuta mtu kwa bidii lakini bado hawajapata mwenza na lazima kuna kitu hakiko sawa kwao kuishi peke yao.

Mawazo haya yote yanatokana na shinikizo la kufuata kanuni za kijami kama vile kukutana na mpenzi, kuolewa, kuwa na watoto wawili au watatu na mbwa na uwe na kila kitu katika maisha ya furaha.

Ingawa watu wamekuwa wakitathmini upya kanuni hizi za kijamii kila mara kwa miongo kadhaa, utafiti wa hivi majuzi unaonyesha kwamba aibu ya kuwa mseja bado inaendelea.

Takwimu kutoka tovuti ya uchumba ya Match, iliyochambuliwa na BBC, inaonyesha kuwa kati ya watu wazima 1,000 wa Uingereza waliohojiwa, 52% walisema wanaona aibu kuwa waseja "tangu kuanza kwa janga", labda kutokana na ukweli kwamba ni ngumu zaidi kujua ni nani unaweza kumhesabia katika hali ya marufuku ya kutoka nje. Na 59% kati yao wanasema "wameridhika na hali yao ya uhusiano", lakini wanabaki kuwa walengwa wa maswali ya kufedhehesha.

Kuendelea kuhukumu dhidi ya watu wasio na wapenzi sio tu ni aibu, lakini pia ni kitu kilichopitwa na wakati katika nchi nyingi.

"Maisha ya Useja yalionekana kama kipindi cha mpito, ambapo watu walipitisha muda hadi walipoolewa au kuolewa tena," Bella DePaulo, mwandishi wa vitabu.

Lakini leo, Bw DePaulo anasema Wamarekani hutumia muda mwingi katika maisha yao ya utu uzima bila kuoa au kuolewa.

Kwamujibu wa sensa ya kitaifa nchini Marekani, mwaka 1970,  40% ya kaya za marekani ziliundwa na wanandoa na watoto wao, wakati 17% waliishi peke yao kama watu wasio na wenza. Na mwaka 2012, 27% ya kaya za Marekani ziliundwa na watu wasio na waume na 20% tu ya wazazi na watoto.

Lakini hata kwa mabadiliko haya ya takwimu, bado ni wazi kutoka katika tafiti kuwa watu ambao hawako katika uhusiano wa kimapenzi wanaendelea kuwa na shida na marafiki na jamaa zao walioolewa na pia wao wenyewe.

Ingawa watu wasio na wapenzi wanaonekana kuzidi kuchagua na kuwajibika kwa hali ya uhusiano wao, shinikizo la kutafuta wapenzi si lazima liondoke.

Lakini kunaweza kuwa na maendeleo fulani, kwani asilimia inayoongezeka ya watu wasio na wapenzi katika idadi ya watu inaweza kuisha  kuzidi unyanyapaa.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika filamu ''The Diary of Bridget Jones'', mhusika mkuu anatathminiwa kuhusu hali yake ya ndoa na si mafanikio yake ya kitaaluma.

Madhara kutokana na fedheha ya kuwa ‘Mseja’

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana na mtaalamu wa magonjwa ya akili Allison Abrams, kutoka New York nchini Marekani, aibu ya kuwa mseja inajumuisha "kumlaumu mtu kwa kutokuwa na mwenzi na kutokubaliana na matarajio ya jamii ya kuoa umri fulani". Ndio maana watu wengine huchukulia watu wasio na wapenzi "tofauti," anaongeza.

"Watu hufikiria kuwa wewe ni mpweke na unachosha ukiwa peke yako," anasema mtaalamu wa programu ya uchumba ya Happn Ipek Kucuk.

Utafiti uliowasilishwa na Match uliuliza ni "misemo ya aibu" ya kawaida inayotolewa kwa watu wasio na wapenzi. Na 35% walisema ni  "mtapata mtu hivi karibuni", wakati 29% walisema"lazima uhisi upweke sana" na 38% walisema watu kwa ujumla wanawapa pole kuhusu kuwa mseja.

Kulingana na DePaulo, maneno yanayowazunguka watu waseja ni pamoja na dhana kwamba walio kwenye ndoa wana ufahamu wa kipekee kuhusu maisha ambayo watu wasio na wapenzi hawana, kwamba maisha ya useja ni "ya kusikitisha" na kwamba kuwa mseja kunamaanisha kuwa na ubinafsi. Na hakika, utafiti unaziunga mkono kama hadithi potofu, ikiwa ni pamoja na utafiti wa Kijerumani wa 2018 ambao uligundua kuwa dhana kuhusu watu wasio na wenzi kuwa hawana furaha na wanandoa ndio wenye furaha si sahihi.

Lakini dhana hizi potofu sio tu mbaya na zinaweza kuwa na madhara.

Kwa mujibu wa mwanasaikolojia Abrams, aibu inayotokana na tabia ya kijamii kwa watu wasio na wenzi inaweza kuharibu taswira yao binafsi. Hata kama mwenyewe haoni aibu na marafiki na wapendwa wake, kushindwa kufikia malengo ya maisha kama vile ndoa na watoto kunaweza kuwa na madhara hasa kwa wale wanaotafuta wenzi kwa bidii  kwa sababu ndivyo jamii kwa ujumla inavyotazamia kutoka kwa watu.

"Mara nyingi nimeona hii kuwa moja ya sababu za msongo wa mawazo," anasema Abrams.

Aibu ya kuwa mseja inatoka kwa vyanzo vingi, kando na marafiki na jamaa zetu 'wadadisi'. Serikali pia zinachangia, kuwapa watu waliofunga ndoa kisheria manufaa mbalimbali ambayo waseja hawawezi kufurahia.

Wengine wanaamini kuwa inatuma ujumbe kuhusu "njia sahihi" ya kuishi maishani, ikitumika kama uimarishaji mzuri kwa watu walioolewa na kuwafanya watu wasio na waume wafikirie kwa urahisi zaidi wazo kwamba wataishi maisha yao ya utu uzima kwa njia sawa, njia mbaya.

Kwa mfano, DePaulo anasema kwamba, Marekani, mfanyakazi anaweza kuongeza mwenzi wake kwenye bima ya afya, lakini waseja hawawezi kufanya vivyo hivyo kwa watu wa maana, kama vile ndugu au marafiki wa karibu. Wanandoa na familia pia hufurahia upendeleo ambao haupatikani kwa watu wasio na wapenzi katika maeneo mengine.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kulingana na kanuni za kijamii, 'kukutana na mwenzi, kuoa, kupata watoto na mbwa' ni kati ya vitu muhimu kwa maisha ya furaha.

"Wasichana wa zamani"

Kama unyanyapaa wowote wa kitamaduni, aibu ya useja haijasambaa kwa usawa. Wanawake huwa wanateseka zaidi na tamaduni zingine huweka mkazo zaidi kwenye ndoa na watoto kuliko zingine.

Kwanza kabisa, angalia jinsi watu wanavyowaelezea wanawake wasio na waume dhidi ya wanaume.

Wanaume wasio na wenza, kwa upande mwingine, wanaitwa "bachelors" kwa Kiingereza, na kwa kawaida hufafanuliwa kama yakufurahisha au kuchekesha (si wa sifa mbaya), wasio na wasiwasi na wanaoishi maisha yao bora, sifa nzuri.

"Kulingana na hekima ya kawaida ambayo inaweza kuwa si ya busara au sahihi - wanawake wana wasiwasi juu ya ndoa kuliko wanaume," DePaulo anaamini. "Kwa hivyo nadhani wanawake wasio na waume mara nyingi huulizwa maswali ya kuudhi kama 'una mchumba?'

Abrams, wakati huo huo, anakumbuka kwamba ana wateja wakike wengi zaidi kuliko wateja wa kiume wanaomshirikisha uzoefu ambao uliwafanya waone aibu kuwa waseja, lakini anabainisha kuwa wateja wake wengi ni wanawake.

"Wanaume wasio na wenza wanaweza pia kutendwa kwa njia ya dharau na kiburi," anaongeza DePaulo, huku watu wakiwaona kama watoto, wasioweza kujitunza au "kupenda sana ngono."

"Nguvu ya namba"

Maana ya neno "single" inabadilika. Wataalamu wengine wanaamini kuwa mabadiliko haya ya kitabia na kitamaduni yanaweza kusaidia kuwafanya watu wasio na wenzi wawe wa kawaida na pengine kupunguza hali ya kuwahukumu.

 Katika miaka ya hivi karibuni, watu wenye ushawishi kwenye mitandao ya kijamii na watu mashuhuri wa kawaida wamezungumza kwa kujivunia kuwa waseja. Mwigizaji Emma Watson, kwa mfano, alielezea hali yake hadharani kama "ameingia ubia na yeye mwenyewe", akiwahimiza wengine kuona kukosa mpenzi kama kitu chanya badala ya hasi.

"Kadiri watu wengi wanavyokubali hali yao ya kuwa waseja, ndivyo watu wengine watakavyojisikia huru kufanya hivyo," Bi Abrams anasema.

Utafiti wa Oktoba 2021, uliofanywa na programu ya Bumble na kuchambuliwa na BBC, ulionyesha kuwa 53% ya zaidi ya watumiaji 8,500 wa programu waliohojiwa nchini Kanada, Ufaransa, Ujerumani, India, Mexico, Ufilipino, Australia, Uingereza na Marekani "wamegundua kuwa ni sawa kuwa single kwa muda" kutokana na covid-19.

Pia, tangu kuanza kwa janga hili, watu wengi wasio na wapenzi wameripoti hisia chanya na maendeleo kuhusu hali yao ya uhusiano. Kulingana na utafiti wa tovuti ya Match dating, 42% ya watu waliohojiwa wanasema "wamefurahia" kuwa waseja wakati wa janga hilo.

Lakini takwimu hii inaonyesha kuwa 58% wengine waliohojiwa hawakuthamini hali hii. Kwa kweli, kutengwa kulikoletwa na janga hili kumeumiza watu wengi wasio na wapenzi na kuongeza aibu kwa wengine.

Kwa hakika, Abrams anapendekeza kwamba aibu kuhusu kuwa mseja “bado imeenea sana,” ingawa idadi inayoongezeka ya watu wasio na wenza katika nchi kama Marekani inaonyesha uwezekano wa kupungua kwa tabia hii.

 Lakini wataalam bado wanatarajia mabadiliko haya ya kitamaduni kuendelea hukumu wasio na wenza. DePaulo anaita mchakato huu "nguvu ya namba," " Ofisi ya Sensa ya Marekani ilipotoa takwimu zake za hivi karibuni, matokeo yalionyesha ongezeko la idadi na uwiano wa watu wasio na wenza."