Mzigo wa akili: Jinsi shukrani inavyoimarisha mahusiano baina ya wenzi

Un homme lave la vaisselle devant une femme qui boit son thé

Chanzo cha picha, LaylaBird

Jumamosi moja asubuhi, mume wangu alishauri nibaki nyumbani ili yeye atoke na watoto.

Nilifarijika sana kwa sababu hua muda mwingi nabaki na watoto, kutokana na mazingira ya kazi zetu.

Nilijua anataka nipate muda wangu binafsi wakujipumzisha, lakini nilihisi kuna umuhimu wa kumwonyesha shukrani kwa alichokifanya, nikaamua kusafisha nyumba na kupika chakula muda ambao alikuwa ametoka.

Shukrani zinajidhihirisha kutokana na jambo jema; kushikamana na jambo linalo waungaisha watu pamoja na pia ambalo husaidia kuwa na mahusiano mazuri.

Lakini pia inakuwa tatizo kwenye mazingira tofauti kama vile nyumbani na kwenye kulea watoto, jambo ambalo huwa huwa sio la haki.

Baada ya kuandika kuhusu Mzigo wa akili ( Fikra za kujificha kwenye upangiliaji kazi ambao hufanyawa zaidi na wanawake kwenye kukamilisha kazi za majumbani) wanawake kumi na mbili majibu yao yalikuwa na neno " kushukuru."

Kuna baadhi walishukuru kwa kuwa wenza wao walikuwa wakiwasaidia na pia kushirikiana, Japo wengine walionyesha kutokuwa na usawa kwenye mambo mengi kwahiyo hawakuona umuhimu wa kuwashukuru wenza wao pale wanaposaidiwa.

Kwahiyo shukrani hujidhihirishaje Majumbani, huku tukijua kuwa kazi zote hufanywa na wanawake kwenye mahusiano baina ya njinsi mbili tofauti?

Kwanini tunawashukuru na kuwasifia wenza wetu wanapo tusaidia kazi ambazo zinatakiwa kufanywa kwa kushirikiana, hivi kuna ulazima wakufanya hivyo?

Kwa yote hayo tunatakiwa kushukuru kwa kazi ndogo tunazo saidiwa, hata kama kazi zote za nyumbani na uleaji wa watoto unakuwa sio sawa, kwa kubaki kwa upande mmoja?

Shukrani inavyoimarisha mahusiano:

Un homme souriant fait le ménage

Chanzo cha picha, Prostock-Studio

Maelezo ya picha, Shukrani ni kitendo cha ubinadamu; Ni hisia zakuonyesha shukrani na kushukuru mtu

Kuna faida nyingi sana kwa mtu anaeshukuru na kwa anaepokea shukrani.

Kazi za zamani za saikolojia ya shukrani, zilionyesha mifano kama nakala za washiriki walionyesha shukrani kwa kuandikiana shukrani kwenye majarida mbalimbali, ambayo yalionyesha ushirikiano mzuri, baadae watafiti mbalimbali waligundua kuwa shukrani huonganisha watu pamoja na hutengeneza muunganiko mkubwa kwenye mahusiano hayo kwa kuridhiana,.

"Watu wanapokuwa wamepata faida flani kutoka kwa mtu mwingine, huwa inabadilisha mtazamo kwenye mahusiano na pia humbadilisha mtu" Alisema Mwanasaikolojia Shelly Gable wa chuo cha Califonia, kilichopo santa barbara.

Shukrani hutumika kwenye mahusiano mapya na yanayoendelea, hutengeneza na kudumisha mahusiano ya karibu kwa watu waliokutana kwa mara moja tu.

Sio lazima shukrani iendane na ukubwa wa zawadi au jambo utakalofanya kwa kushukuru.

Kwenye moja ya funzo kuhusiana na Shukrani, huonyesha kuwa ni hali ya kuelewana na kuthaminiana na huleta hisia za shukrani zaidi ya kushukuru kwa kutoa zawadi au kitu chenye thamani inachopokelewa na mtu wengine kama shukrani.

"Kuna njia nyingine nyingi za kupewa shukrani ambayo unaihitaji na utakayo ifurahia" Alisema Gable Kwahiyo shukrani ni tendo ambalo huonyesha viashiria kuwa mtu mwingine anafanya jitihada za kutuelewa.

Japo kuwa haitoshi kumshukuru mtu kimya kimya pale ambapo amekufanyia kitu

Gable kushirikiana na Sara Algoe kwenye utafiti kuhusiana na shukrani, wanaelezea kuwa tunatakiwa kuonyesha hisia zetu kwenye mahusiano ili tuweze kufaidika, shukrani isipo onekana baina ya watu wawilli inaweza kuathiri mahusiano yao.

Une femmes Bassari avec foulard transportant de l'eau d'un puits.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kushukuru kunatofuautiana kulingana na jinsia;

Utafiti unaonesha kuwa mwanamke huwa anashukuru zaidi ya mwanaume Jeffrey Froh, profesa wa saikolojia katika chuo cha Hofstra kilichopo Marekani, anaeleza kuwa wanawake ninwepesi kuzoea mazingira ya jamii flani na pia hisia za karibu sana.

Kiukweli Mafunzo haya yanaonyesha kuwa mwanamke anauwezo wa kuonyesha hisia nzuri kuliko mwanaume na pia wana uwezo wa kuonesha hisia zaidi zaidi za hasira.

Watafiti wengine wanaelezea kuwa wanawake wenye madaraka ( hasa wale wenye kipato cha juu) huonyesha shukrani kwa kiasi kidogo sana, na pia wanaume ndio wenye kiwango kikubwa cha kipato kwa watu waliopo kwenye mahusiano Marekani , kulingana na kituo cha utafiti cha Pew( kwa kutumia data kuanzia 2017)

Mazingira ya Familia isiyo na usawa

Une femme dans une cuisine

Chanzo cha picha, Getty Images

Faida moja kubwa ya shukrani ni kumshukuru mwenza wako wa kumuonyesha, na huleta hamasa ya kuzidi kufanya jambo shukrani kwenye upande wa mahusiano ya mgawangiko wa kazi za ndani ya nyumba huwa ni changamoto pasipo kuwa na mgawanyiko wa kazi kwa usawa.

Ni ukweli usiofichika kuwa mwanamke ndio anaobeba mzigo wa akili kwenye kufanya au kupangilia kazi za nyumbani , lakini pia kuna mgawanyo wa kazi za nyumbani usio na haki.

Kama mmoja atafua nguo basi mwingine akionyesha shukrani kwa mwenzake kwa anachokifanya itasaidia kumpa nguvu za kuzidi kufanya hizo kazi mara kwa mara.

Kwenye mahusiano ya jinsia mbili tofauti, wenye watoto mwanamke ndio anaebebeshwa majukumu yote ya nyumbani, wawe wamekubaliana au hawajakubaliani, ila nimtazamo ambao mwanamke anachukuwa kuwa ndio mwenye kubebesha mzigo wa Akili kwa kushughulikia kazi zote za nyumbani.

Inaendelea kuwa mwanaume hawezi kumshukuru Mwanamke kwa kazi anazozifanya wala mwamke hawezi kumshukuru mwanaume kwa kazi ambazo anazifanya, kwa mazingira haya huweza kusababisha mahusiano kuvunjika hasa pale mwanamke anapoonekana kama mtu anawajibika na ulezi wafamilia na pia kama kijakazi wa kazi zote za nyumbani.