Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 16.04.2022: Nunez, Jorginho, Tchouameni, Azpilicueta, Phillips

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle wametoa kwa Benfica euro 60m (£50m) kwa mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 22, kujaribu kuzuia foleni ya wapinzani wa Premier League wanaowania kumsajili. (Footmercato - in French)

Kocha Maurizio Sarri anatamani kuungana tena na Jorginho huko Lazio, huku kiungo huyo wa kati wa Italia, 30, akiwa hana uwezekano wa kupewa kandarasi mpya na Chelsea baada ya 2023. (90min)

Meneja anayekuja wa Manchester United Erik ten Hag anamtaka kiungo wa kati wa Monaco na Ufaransa Aurelien Tchouameni na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 anapendelea kuondoka Ligue 1. (ESPN)

Arsenal wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Hoffenheim na Austria Florian Grillitsch, 26, kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Telegraph, via Metro)

Leeds United imeungana na Arsenal na Newcastle United kuonyesha nia ya kutaka kumnunua Grillitsch. (Mail)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26, anataka kusalia Leeds na atakataa ombi la Manchester United kwa kusaini mkataba mpya. (Sun)

Tottenham watakuwa kwenye soko la kutafuta beki wa kati wa upande wa kushoto msimu huu wa joto na wanafuatilia hali ya mlinzi wa Uhispania Mario Hermoso, 26, huko Atletico Madrid. (Mail)

Borussia Dortmund wameafikia makubaliano ya kimsingi na Red Bull Salzburg kuhusu kumsajili Karim Adeyemi lakini fowadi huyo wa Ujerumani, 20, bado yuko kwenye mazungumzo na Liverpool, RB Leipzig na Paris St-Germain. (Sky Sport Germany - in German)

Manchester United walikuwa na skauti kwenye ushindi wa RB Leipzig wa Ligi ya Europa Alhamisi kumtazama mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 24, ambaye alifunga mabao mengine mawili na kufikisha 30 msimu huu. (Nicolo Schira, Twitter)

th

Chanzo cha picha, VISIONHAUS

Kipa chaguo la pili wa Chelsea Mhispania Kepa Arrizabalaga, 27, analengwa na Juventus. (Fichajes - in Spanish)

Tottenham wana uhakika wa kupata ofa ya kumnunua mlinda mlango wa West Bromwich Albion anayecheza na timu ya taifa ya Uingereza Sam Johnstone, 29, licha ya kutakiwa na Manchester United(Express)

Barcelona wameongeza kasi katika kumsaka nahodha wa Chelsea Cesar Azpilicueta, 32, huku beki huyo wa Uhispania akishinikiza kuondoka huku kukiwa na hali ya sintofahamu ya kifedha huko Stamford Bridge. (Sport - in Spanish)

Paolo Dybala, 28, anapanga kufanya mazungumzo na Arsenal na Tottenham huku kandarasi ya mshambuliaji huyo wa Argentina katika klabu ya Juventus ikitarajiwa kumalizika msimu wa joto. (Express, via Corriere Dello Sport)

Vilabu vingi vya Ulaya na Premier League vinajipanga kumpiga bei beki wa kati wa Torino raia wa Brazil Gleison Bremer, huku Arsenal, Leicester, Everton na Newcastle wakiwa wamewasiliana na klabu hiyo ya Serie A. Tottenham na Atletico Madrid wametuma maskauti huko Turin, na Bayern Munich na Borussia Dortmund pia wanamfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. . (Gazzetta Dello Sport - in Italian)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa kati wa Ubelgiji Eden Hazard, 31, hataki kuondoka Real Madrid msimu huu wa joto, licha ya Arsenal, AC Milan na Borussia Dortmund kutajwa kuwa wanunuzi. (RTBF, via RTL Sport - in French)

Manchester City bado wanamfuatilia Erling Braut Haaland, 21, lakini wangependelea kuepuka kuamsha kipengele cha kutolewa cha mshambuliaji huyo wa Norway cha pauni milioni 63, ambacho watalazimika kulipa kwa mkupuo mmoja. Badala yake wanataka kukubaliana dili na Borussia Dortmund ambalo litawafanya kulipa fedha zaidi lakini kufanya malipo zaidi ya mara moja. (90min)

Beki wa The Gunners wa Brazil Gabriel Magalhaes, 24, anasema anafuraha na ameangazia taaluma yake huko Emirates, huku kukiwa na tetesi za kutakiwa na Barcelona. (Fabrizio Romano)

Fenerbahce na Galatasaray wanataka kumsajili James Rodriguez wa Al Rayyan msimu huu wa joto lakini winga huyo wa Colombia, 30, ana nia ya kujiunga na Atletico Madrid. (FotoMac, via Mundo Deportivo - in Spanish)