Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 09.04.2022: Salah, Dembele, Haaland, Bowen, Pepe, Hazard, Ozil

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Liverpool Mmisri Mohamed Salah anasema sio muda unafaa kuzungumzia kuhusu mazungumzo ya mkataba wake yanayoendelea na klabu yake, ambayo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 ameyaeleza kama "hali ya siri". (Sky Sports)
Newcastle wanania ya kusaini mkataba na Muingereza Jarrod Bowen mwenye umri wa miaka 25 ambaye anachezea klabu ya West , safu ya mashambulizi. (90min)

Chanzo cha picha, Reuters
Barcelona ainamini winga Mfaransa mwenye umri wa miaka 24, Ousmane Dembele, ambaye atakuwa huru katika msimu wa kiangazi, atajiunga na Paris St-Germain kama mshambuliaji Kylian Mbappe, 23, ataondoka katika klabu hiyo ya Ufaransa. (El Nacional - in Catalan)
Manchester City na Real Madrid kwa pamoja zinamtaka kiungo wa kati wa England na Borussia Dortmund Jude Bellingham, 18. (Fichajes - in Spanish)

Chanzo cha picha, Reuters
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, raia wa Norway mwenye umri wa miaka 21 Erling Braut Haaland anahofia kwamba Manchester United haitaweza kufikia viwango vya matamanio yake uwanjani wakati akifikiria uwezekano wah atua inayofuata kimchezo. (ESPN)
Mshambuliaji wa Benfica Darwin Nunez, 22, amethibitisha kuwa anawabadilisha mawakala wake kabla ya msimu wa uhamisho wa majira ya kiangazi, huku ikisemekana kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uruguay huenda akajiunga na klabu za Primia Ligi Arsenal na Manchester United. (Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanajiandaa kumuuza winga Muivory Coast Nicolas Pepe, 26 kwa euro milioni 30 (£25m). (Calciomercato - in Italian)
Newcastle wako tayari kumhamisha kiungo wa safu ya kati wa Leeds Kalvin Phillips. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 wa timu ya kimataifa ya England pia amehusishwa na Manchester United. (The I - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
The Gunners pia wamefanya mkutano na Real Madrid juu ya uwezekano wa kusaini mkataba wa mkopo na mshambuliaji mbelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 31. (Foot Mercato - in French)
Aston Villa wanamfuatilia kwa karibu winga Muingereza wa PSV mwenye umri wa miaka 20 Noni Madueke. Leicester City pia wanamtaka. (Talksport)
Tottenham na Tanguy Ndombele hatarajii Lyon kuchukua chaguo la kugeuza mkopo wa kiungo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 katika klabu ya Ligi 1 na kuufanya mkataba wa kudumu wa thamani ya pauni milioni 54 . (Evening Standard)
Hatahivyo, Spurs wanajiandaa kwa ajili yad au la mlinzi wa Peterborough United Muingereza Ronnie Edwards mwenye umri wa miaka 19. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Kiungo wa kati wa Fenerbahce Mjerumani Mesut Ozil
Kiungo wa kati wa Fenerbahce Mjerumani Mesut Ozil, 33, anaweza kujiunga na MLS upande wa Inter Miami. (Metro)
Uongozi wa Everton hauamini kwamba kumfuta kazi meneja Frank Lampard kutaboresha matarajio yao ya kuepuka kuenguliwa kutoka Primia Ligi katika hatua hii . (Sky Sports)
Manchester United na Real Madrid wamewasiliana na Everton kuhusu uwezekano wa kusaini mkataba na mshambuliaji Mbrazil Richarlison, 24. (Sport Witness)
Mshambuliaji wa zamani wa Uholanzi na Manchester United Robin van Persie, ambaye ni kocha katika Feyenoord, amekataa fursa ya kujiunga na wakufunzi wa Erik ten Hag katika Old Trafford. Meneja wa Ajax Ten Hag ndiye anayependelewa zaidi kuwa meneja mpya wa Manchester United . (Soccer News - in Dutch)












