Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 23.02.2022: Felix, Mbappe, Mane, Cavani, Dybala, Martinez, Olise, Nkunku, Johnson

Joao Felix

Chanzo cha picha, Angel Martinez/getty images

Maelezo ya picha, Joao Felix

Arsenal wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 22, kutoka kwa mabingwa wa Uhispania Atletico Madrid. (El Chiringuito, via Mail)

Matumaini ya The Gunners kumsajili mchezaji Sergi Roberto kutoka Barcelona yameongezeka kwani mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania mwenye umri wa miaka 30 bado hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Catalan. (Sun)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid bado wana uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, kwa uhamisho wa bila malipo kutoka Paris St-Germain na wanapanga kutangaza mkataba huo mwishoni mwa msimu huu. (Goal)

Iwapo klabu hiyo ya Uhispania itashindwa kumsajili Mbappe na fowadi wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 21, basi wataelekeza mawazo yao kwa mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 29 na Senegal Sadio Mane. (Fichajes - in Spanish)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambulizi wa Manchester United wa Uruguay Edinson Cavani, 35, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu, anasemekana kuwa tayari kusikiliza ofa kutoka kwa klabu ya Botafogo ya Brazil. (Goal)

Mchezaji wa RB Leipzig Christopher Nkunku atagharimu Manchester United "angalau euro 75m" ikiwa wataendelea na juhudi za kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24. . (Bild - in German)

Newcastle na Aston Villa wangeongoza mbio za kumnasa Joe Gomez iwapo Liverpool itaamua kumuuza mlinzi huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 msimu huu. (Athletic - subscription required)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham wamejitokeza na "ofa thabiti zaidi" ya kutaka kumsajili mshambuliaji Paulo Dybala, 28, kutoka Juventus msimu wa joto, lakini Barcelona na Inter Milan zinasalia kuwa chaguo la Muargentina huyo. (Sport - in Spanish)

Crystal Palace wanakabiliwa na pambano la kutaka kumbakisha mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 18, Michael Olise, 20, ambaye anasakwa na Arsenal, Chelsea na Everton pamoja na Bayern Munich na Lille. (Sun)

Liverpool wanatarajiwa kuanzisha upya nia ya kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 24, ambaye mabingwa hao wa Italia wameripotiwa kuwa na thamani ya euro 90m. . (Calciomercato - in Italian)

Nottingham Forest imeanza mazungumzo ya kandarasi na winga wa Wales Brennan Johnson mwenye umri wa miaka 20 kwa nia ya kuzuia leongo la Brentford, Crystal Palace na West Ham. (Standard)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal wako tayari kumpa meneja Mikel Arteta mkataba mpya wa miaka mitatu msimu huu wenye thamani ya £25m. (Sun)

Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Savio kutoka Atletico Mineiro, kabla ya kumpeleka kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 kwa PSV Eindhoven. (Voetbal International - in Dutch)