Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 11.02.2022:Ronaldo, Rice, Mane, Kessie, Tielemans, Saka

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anapanga mazungumzo na wakala wake kuhusu mustakabali wake wa Manchester United baada ya kukatishwa tamaa na maisha huko Old Trafford. (Star)
Kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, ambaye analengwa na Chelsea na Manchester United na City, amesisitiza nia yake ya kushinda mataji na kucheza Ligi ya Mabingwa, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliwatuliza mashabiki wa West Ham kwa kuelezea uvumi juu ya hatma yake kama "kelele tu". (Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images
Paul Pogba atalazimika kulipa posho kwa kandarasi kubwa ya mwisho ya maisha ya kiungo huyo wa kati wa Manchester United na Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 ikiwa anataka kukamilisha ndoto yake ya uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Mirror)
Mlinda mlango wa Chelsea mwenye thamani ya pauni milioni 72 Kepa Arrizabalaga, 27, anaweza kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa joto huku The Blues wakiwa hawajapanga kumzuia mchezaji huyo wa Uhispania ikiwa anataka kuondoka. (Sun)
Barcelona wanashinda mbio za kumsajili kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia analengwa na Liverpool. (Marca)

Chanzo cha picha, GEOFF CADDICKt
Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, 29, yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo ya Anfield huku Barcelona na Real Madrid wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal. (Goal, via Mirror)
Leicester City wamepunguza dau la kumnasa Youri Tielemans, 24, kutoka pauni milioni 60 hadi pauni milioni 35, huku Arsenal na Manchester United wakiwa katika mbio za kumnunua kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji msimu huu. (Het Nieuwsblad,via Metro)
Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amekiri kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu huu kunaweza kuwa muhimu katika kumfunga winga wa Uingereza Bukayo Saka, 20 - ambaye anahusishwa na Liverpool - kwa kandarasi mpya. (Express)
Mlengwa wa Manchester United Manuel Akanji anataka kuongeza mishahara yake maradufu huku Borussia Dortmund wakiweka bei wanayohitaji kumnunua mlinzi huyo wa Uswizi, 26. (Bild, via The Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkufunzi wa Uhispania Luis Enrique, 51, ameibuka kuwa mgombea wa kushtukiza kwenye kibarua cha kocha wa Manchester United. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa Uhispania Cesar Azpilicueta anataka kuzungumza na Chelsea kuhusu mustakabali wake, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akihusishwa na kuhamia Barcelona mkataba wake utakapokamilika msimu wa joto. (Mundo Deportivo)
Barcelona wanataka kusajili mabeki wa bajeti na pia wako tayari kumuuza mlinzi wa kulia wa Marekani Sergino Dest, 21, ili kusaidia kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Haaland, 21.(ESPN)
Tottenham wanapanga kuelekeza zaidi mkakati wake wa uhamisho kwa vijana wenye vipaji vijavyo na wale walio kwenye kandarasi zinazoelekea ukingoni, huku kiungo wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 18 Mamadou Coulibaly - ambaye yuko Monaco - akifikiriwa. (Mail)
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski anataka kuhamia Real Madrid, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 anaweza kuona hilo lingekuwa jambo la kipumbavu ikiwa timu hiyo ya Uhispania itamsajili Haaland wa Dortmund. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal Alexis Sanchez, 33, anatazamiwa kuongezewa mkataba mpya na Inter Milan, lakini raia huyo wa Chile atalazimika kukatwa mshahara. (Gazzetta dello Sport)
Arsenal wamekamilisha makaratasi ya kumsajili mlinda mlango Mmarekani Matt Turner mwenye umri wa miaka 27 kutoka New England Revolution kwa pauni milioni 7.5. (Mail)












