Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 09.02.2022: Kane, Mane, Xhaka, Tielemans, Kean, Vidal, Kelly

Chanzo cha picha, Reuters
Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 29, atakuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto ikiwa Real Madrid au Barcelona watamnunua. (Goal in Spanish)
Nahodha wa Uingereza Harry Kane 'ana furahishwa sana' na mkufunzi wa Tottenham Antonio Conte na, wakati Spurs wanamtaka mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 abaki katika klabu hiyo, naye hajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake. (Fabrizio Romano,via Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Roma wanatarajiwa kufanya jaribio jipya la kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Uswizi Granit Xhaka, 29, msimu huu. (football.london)
Manchester United inamfuatilia kiungo wa kati wa Leicester City na Ubelgiji Youri Tielemans, 24, mwenye thamani ya pauni milioni 40. (Star)
Vilabu kadhaa vya juu vya Ligi ya Primia, pamoja wa wasomi wa Uropa, wamemtazama mshambuliaji wa Reims, Hugo Ekitike. Newcastle United ilishindwa kumsajili Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 19 mwezi Januari. (90 min)

Chanzo cha picha, PA Media
Paris St-Germain wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Italia Moise Kean katika majira ya joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 yuko kwa mkopo Juventus kutoka Everton na timu hiyo ya Serie A ina wajibu wa kufanya uhamisho wake kuwa wa kudumu kwa pauni milioni 23.6, pamoja na pauni milioni 2.5 kama nyongeza. (Calciomercato,via Football Italia)
Newcastle United wanajiandaa kumnunua mlinzi wa Bournemouth Muingereza Lloyd Kelly, 23, bila kujali kama watashuka daraja. (Football Insider)
Tottenham Hotspur wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan na Chile Arturo Vidal, 34. (La Latercera, in Spanish)
Norwich City na Rangers wanamtazama mlinda mlango wa Schalke raia wa Austria Martin Fraisl, 28, ambaye kandarasi yake itamalizika msimu wa joto. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric, 36, amependekeza kwamba anaweza kuendelea kucheza hadi atakapofikisha umri wa miaka 40. (Marca).
Mike Ashley bado anataka kununua klabu ya Championship ya Derby County lakini anatambua kwamba muda unasonga. (Star)













