Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 08.02.2022: Mbappe, Rice, Sule, Benzema, Traore, Raphinha

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Ufaransa Karim Benzema, 34, ametaka kukutana na rais wa Real Madrid Florentino Perez mwezi Machi huku akihofia kuwa huenda akapoteza nafasi yake katika timu ikiwa mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, atahama msimu huu. (Onze - in French)
Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe amekuwa akihusishwa na kuhamia Real Madrid wakati kandarasi yake ya Paris St-Germain itakapokamilika msimu wa joto lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anasema hajafanya uamuzi kuhusu mustakabali wake. (Amazon Prime, via Mirror)
Kocha wa West Ham David Moyes anafikiri Declan Rice, 23, ana thamani ya zaidi ya pauni milioni 100, huku Manchester United, Chelsea na Manchester City zote zikihusishwa kutaka kumnunua kiungo huyo wa kati wa England msimu wa joto. (Metro)
Chelsea imepata pigo baada ya Niklas Sule, 26, kukubali kujiunga na Borussia Dortmund msimu wa joto wakati beki huyo wa Ujerumani akiondoka Bayern Munich. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wamekabiliwa na kipingamizi katika harakati zao za kumnunua Christopher Nkunku, 24, baada ya RB Leipzig kusisitiza kuwa mchezaji huyo anayesakwa na Ufaransa atasalia nje kwa angalau msimu mwingine. (Sky Sport Germany)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wamekubali ada ya £12m kwa mauzo ya kudumu ya kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira, 26, kwenda Flamengo. (Universo,via Sun)
James Garner ana matumaini ya kusalia Manchester United msimu ujao huku kiungo huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 20 akikaribia miezi ya mwisho ya muda wake wa mkopo na Nottingham Forest. (Manchester Evening News)
Mkufunzi wa Wolves Bruno Lage amemuunga mkono winga Mhispania Adama Traore, 26, kupata uhamisho wa kudumu wa pauni milioni 29 kwenda Barcelona kufuatia mchezo wake wa kwanza kurejea Uhispania. (Mirror)
Lage anataka kuongeza mtu anayelengwa kwenye kikosi chake cha Wolves katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi. (Birmingham Live)
Mkufunzi wa Leeds United Marcelo Bielsa ametetea klabu hiyo kutosajili mchezaji mkuu mwezi Januari na kuongeza kuwa ilikuwa "ya thamani sana" kwa upande wa Elland Road "iliweza kuwafanya wachezaji kusakwa na timu zingine". (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Leeds United hawakufurahia kumuuza Raphinha, 25, mwezi Januari lakini wanatarajia kuvutiwa na winga wa Brazil, kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 26 na mlinda mlango wa Ufaransa Illan Meslier, 21, wakati wa majira ya joto. (Athletic)
Beki wa kushoto wa Ujerumani Robin Gosens, 27, anasema alizingatia ofa kutoka Newcastle United kabla ya kuchagua kujiunga na Inter Milan kutoka Atalanta mwezi Januari. (Kicker -in German)
Everton na Leicester City, pamoja na vilabu vingine kadhaa vya Ligi ya Primia, vinamfuatilia kiungo mshambuliaji wa Bristol City na England wa chini ya miaka 19 Alex Scott. (Football Insider)












