Tetesi za soka Ulaya Jumatano 24.11.2021: Pochettino, Zidane, Ziyech, Werner, Haaland, Trippier, Origi

Manchester United wako tayari kuacha utafutaji wa meneja wa muda wa klabu hiyo iwapo wanaweza kumpata Mauricio Pochettino kutoka Paris St-Germain sasa. (Guardian)
Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, ambaye ana uwezekano mkubwa wa kulengwa na Manchester United anataka kuchukua umeneja katika PSG iwapo Pochettino anaondoka kuelekea Old Trafford. (Telegraph - subscription required)
Meneja wa zamani wa United Sir Alex Ferguson, ambaye ni Mkurugenzi wa bodi ya soka ya klabu hiyo, hatakuwa na jukumu lolote katika kumsaka meneja wao mpya. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool, Leicester na Newcastle wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Guinea Aguibou Camara mwenye umri wa miaka 20, anayecheza katika klabu ya Olympiakos. (Sun)
Borussia Dortmund wana andaa mkataba mpya kwa ajili ya mshambuliaji Erling Braut Haaland, 21, katika azma ya kumshawishi mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway kuendelea kubaki katika klabu hiyo. (Sky Deutschland, in German)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wanamtafuta mchezaji wa wa kimataifa wa Morocco anayechezea klabu ya Chelsea Hakim Ziyech, 28, na mshambuliaji Mjerumani Timo Werner, 25, kama wachezaji mbadala kwa mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 26. (ESPN)
Newcastle wana nia na kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Axel Witsel, 32, na mchezaji wa kimataifa wa ubelgiji, ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu-yuko tayari kuhama. (Sport1, in German)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji Mbelgiji mwenye umri wa miaka 26 Divock Origi, ambaye analengwa na Newcastle, hataruhusiwa kuondoka Liverpool mwezi Januari. (Northern Echo)
The Magpies (Wachawi) hao wanamtaka beki Kieran Trippier, 31, kutoka Atletico Madrid. (Mirror)

Chanzo cha picha, Reuters
Gerrard anataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya Kati-nyuma Pau Torres, 24, kutoka Villarreal. (Fichajes - in Spanish)
Lakini Torres, ambaye alikataa uhamisho ambao ungemlipa milioni 60 (£50.4m) iwapo angehamia Tottenham msimu huu, anafurahia kubaki katika klabu yake ya nyumbani kwa sasa. (Guardian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja mpya wa Aston Villa Steven Gerrard ameidhinisha mauzo mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso Bertrand Traore, 26. (Football Insider)
Mkufunzi wa klabu ya Sevilla Julen Lopetegui, 55, ameutaja uvumi unaomuhusisha na klabu ya mchester United kuwa mbaya (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Liverpool na Uhispania Thiago Alcantara, 30, amepuuzilia mbali uvumi unaomuhusisha na kurudi tena katika klabu yake ya kwanza Barcelona. (Liverpool Echo)
Mchezaji wa kati wa Arsenal na Uswiss Granit Xhaka, 29, atakuwa na nia ya kurejea Borussia Monchengladbach wakati mkataba wake utakapomalizika mwaka 2024. (Mit Geredet, via Mail)

Burnley, Brighton, Norwich, West Brom, Sheffield United na Blackburn zote zinamkodolea macho mshambuliaji Muingereza Rhys Healey, 26, anayechezea klabu ya Ligi ya 2 ya Toulouse. (Team Talk)
United italazimika kulipa Yuro Milioni 10 (£8.4m) iwapo wanataka kumnunua raia wa Argentina Pochettino mwenye umri wa miaka 49 kutoka klabu ya PSG.. (Mirror)












