Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 23.11.2020: Yazici, Henderson, Messi, Giroud, Eriksen, Wilder

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal imepigwa jeki katika harakati zake za kumsajili kiungo wa kati wa Uturuki Yusuf Yazici baada ya ajenti wake kukiri kwamba mchezaji huyo huenda akaondoka katika klabu ya Lille. Mchezaji huyo amefananishwa na kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil 32. (Mirror)
Kipa wa klabu ya Manchester United Dean Henderson, 23, atafuatilia uhamisho wake wa mkopo ili kuimarisha hadhi yake katika kushiriki kombe la mabingwa Ulaya huku klabu za Leeds na Brightong zikihusishwa na ununuzi wa mchezaji huyo mwezi Januari.. (Sun)
Manchester City imesitisha harakati zake za kutaka kumsajili mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, 33, kulingana na mtaalamu wa soka wa Uhispania Semra Hunter. (Sky Sports)

Mshambuiaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, amekiri kukosa muda wa kushiriki katika mechi Chelsea kunamtia wasiwasi na kwamba huenda akafanya maamuzi kuhusu hatma yake ya siku zijazo mwezi Januari. (Mirror)
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 28, yuko huru kuondoka Inter Milan mwezi Januari , afisa mkuu wa klabu hiyo ya Itali Beppe Marotta amethibitisha. (Goal)
Manchester United huenda ikamuwania Eriksen. (Corriere dello Sport, via Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chris Wilder, ambaye klabu yake ya Sheffield United ipo chini ya jedwali la ligi ya premia ikiwa na pointi moja pekee anasisitiza kwamba haogopi kufutwa kazi. (Sky Sports)
Jeraha la mguu la beki wa Barcelona na Uhispania Gerard Pique, 33, huenda likabadilisha jinsi klabu hiyo itakavyomtafuta beki mwengine mwezi Januari kujaza pengo lake. Mabingwa hao wa Catalan wana hamu ya kumsajili beki wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 19. (Manchester Evening News)
Pique ataulizia ushauri mwengine kuhusu jeraha lake kutoka kwa Daktari Ramon Cugat , mtaalamu wa kutibu magoti mjijni Barcelona. (Sport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Katibu wa kwanza wa kiufundi wa klabu ya Barcelona Ramon Planes atakutana na kocha mkuu Ronald Koeman ili kujadili kuhusu usajili wa beki (Marca)
Kiungo wa kati wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 21, amehusishwa na uhamisho kuelekea Tottenham na anakiri angependelea uhamisho wa kujiunga na klabu kuu ijapokuwa anafurahia kusalia katika klabu. (Football London)
Kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 21, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Hertha Berlin, anadai kwamba amepata motisha aliyopoteza chini ya mkufunzi Mikel Arteta akiwa Arsenal. (Telefoot, via Star)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa West Ham na Uingereza Declan Rice amekiri kwamba kuachiwa na Chelsea aiwa umri wa miaka 14 kulimfaidisha kama mchezaji na mtu binafsi. (Football London)












