Gerardo Bedoya: Hadithi ya mchezaji 'mchafu zaidi' duniani

Chanzo cha picha, Getty Images
"Anapoonekana katika runinga, mtangazaji hubeba kadi yake nyekundu mfukoni kwasababu hiyo ndio sifa yake Bedoya zaidi ya chochote kile.
Akiwa mkaazi wa mji mkuu wa Bogota, nchini Colombia, mwandishi wa kandanda Carl Worswick sio mgeni kwa sifa zilizoachwa na Gerardo Bogota. Bedoya 44 ndie mchezaji aliepewa kadi nyingi nyekundu katika historia ya soka.
Kabla ya kwenda nyumbani kwake ili kumfanyia mahojiano, tulirekodi kanda ya video ya mchezo wa Matador kuelezea alivyo yeye binafsi , lakini ni tofauti ya vile ungelitaraji, Worswick, wakati huo akifanya makala ya Futboll Mundial, aliambia BBc Sport.
''Anaonesha kwamba yeye ni mtu tofauti akiwa uwanjani na nje ya uwanja. Alikua mchezaji mwenye heshima lakini hilo halikutosha kumuondoa katika mambo mengine ya kazi anayofanya. Vichwa vya habari mara kwa mara vilisema, ''Mchezaji mchafu zaidi duniani'' akijulikana kama jenerali, Bedoya alipokea kadi 45 nyekundu wakati akicheza kwa muda wa miaka 20 huku kadi nyengine nyekundu akipewa katika chumba cha maandalizi.
Alipokea kadi ya kwanza nyekundu kama naibu kocha baada ya dakika 21 mwaka 2016.
Pengine kadi inayokumbukwa sana ni ile ya 41 aliopewa baada ya kupatikana na hatia kwa kumpiga kisukusuku mchezaji mwengine ambaye baada ya kuanguka alimpiga teke suala lililomfanya kupigwa marufuku kutoshiriki mechi 15.
Licha ya kuwepo kwa ushahidi kuonesha kivingine, Bedoya alisema kwamba huwa 'hayuko anavyodhaniwa' baada ya mechi kukamilika.
''Alikuwa na hasira mbaya'' , aliongezea Worswick.
Wakati alipoona kadi nyekundu hakuweza kujidhibiti. Kutolewa uwanjani dakika 21 katika mechi yake ya kwanza kama naibu kocha - hilo lilipotokea wachezaji wa ziada walikuwa wakicheka, hawakuamini. walijua kwamba itatokea. Ukweli ni kwamba tabia yake haijamsaidia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Akiwa mzaliwa wa eneo la Ebejico 1975, kulikuwa na mengi yaliozunguka maisha yake kama mchezaji wa kandanda ikiwemo kadi nyekundu nyingi alkizopewa.
Zaidi ya yote hayo, alikuwa mmoja ya wachezaji wa timu ya Colombia ilioshinda taji la Copa America la 2001 , ambapo shambulio lake nje ya eneo hatari liliisaidia Colombia kuishinda Honduras katika nusu fainali. Baadaye waliilaza Mexico 1-0 katika fainali.
Mwaka huohuo, goli lake la dakika ya 86 akiichezea klabu ya Argentina ya Racing dhidi ya wapinzani wao River Plate - linakumbukwa kama goli lililosherehekewa sana ambapo liliisaidia Racing kupanda jedwali la ligi na kushinda ubingwa wa Apertura. Lilikuwa taji la kwanza la Racing katika kipindi cha miaka 35.
Akiziwakilisha klabu 13 za Kusini mwa America na katikati , Bedoya alivutia wengi hatua iliomwezesha kujiunga na klabu nyengine ya Boca Juniors na Puebla nchini Mexico , lakini alisalia Colombia katika kipindi kirefu cha uchezaji wake.
Akiwa huko aliisaidia klabu ya Independiente Santa fe kushinda taji lake baada ya miaka 37 mwaka 2012.
Akiwa Santa Fe, mashabiki walimpenda kwasababu alikuwa mchezaji ambaye angevamia na kuwapokonya mpira wapinzani na kutoa huduma yake kwa asilimia 100, alisema Worswick. Wanamuona kama mtu ambaye alijitolea kwa hali na mali .
Bedoya aliheshimiwa na kufunga magoli mazuri , lakini anahisi anakumbukwa kwa kadi nyekundu alizopewa. Kwa Upande wa Santa Fe na mashabiki wa Racing, atakumbukwa kama kiungo muhimu aliyemaliza subra ya kushinda mataji dhidi ya timu kubwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Baada ya Bedoya kushinda taji lake la kwanza kati ya matatu katika klabu ya Deportivo Cali 1998 na kuweka rekodi ya kupokea kadi 14 nyekundu katika kipindi hicho , vituko havikuwa mbali
Alipokea kadi nyengine nyekundi akiichezea Racing huku akiwa amepokea kadi nyengine kati ya saba na nane wakati alipokuwa akicheza klabu hizo za Bogota wapinzani Millonarios na Santa fe mtawalia.
Mchezaji mwenza wa zamani katika Millonarios kati ya 2007 na 2010 , winga wa Colombia Omar Vasquez mara kwa mara walikuwa wakikaa na Bedoya kabla ya siku ya mechi.
''Sio jambo lisilo la kawaida kwa jamii yetu kuwakumbuka watu kwa mambo mabaya, ni lazima akumbukwe kama mchezaji bora wa taifa letu'', Vasquez aliambia BBC Sport.
''Bedoya alikuwa mshindi , mtu alieweka historia ambaye alichezea timu na kushinda mataji na timu bora nchini Argentina na Colombia. Kwangu mie ilikuwa furaha kubwa kuwa katika chumba cha maandilizi naye , na mtu ambaye alipata mafanikio makubwa katika kipindi chake cha uchezaji''.
Rekodi ya dunia iliowekwa na Bedoya haionekani ikivunjwa hivi karibuni. Huku kukiwa na wale walio na fursa ya kuipiku rekodi yake, beki wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos ndie mchezaji wa karibu kuifikia rekodi hiyo baada ya kupokea kadi nyekundu ya 26 dhidi ya klabu ya Manchester City katika kombe la klabu bingwa Ulaya mnamo mwezi februari.
Akiwa na umri wa miaka 34, haiwezekani kwamba huenda akaikaribia. Iwapo Bedoya mwenye umri wa miaka 44 atapatiwa fursa nynegine kurudi kama kocha na hivyobasi kuongeza idadi ya kadi zake nyekundu ni suala ambalo linatarajiwa kuonekana.
Yeye husema kwamba kwa sasa hana maadui, alisema Worswick.
Tangu alipostaafu amekuwa mtu mtulivu ili kujaribu kuandikisha historia yake . Anaamini alitoa huduma yake ka asilimia 100 na kwamba mashabiki walimpenda. Kwa wengi nje ya Colombia , Bedoya Bedoya atasalia kuwa mchezaji wa kandanda mwenye takwimu zilizo na kanda za video za mchezaji rafu na mtu mwenye hasira.
Lakini kwa mashabiki wa Racing na Santa Fe, pamoja na wachezaji wenza atakumbukwa zaidi ya matukio hayo. Alikuwa kiongozi dhabiti na mtu aliyepigania kila mpira, alikuwa akiiongoza timu. Alikuwa mtu mwenye hisia nyingi ambaye angewasaidia wenzake.
''Inaonekana kinyume na alivyo binafsi , lakini akiwa uwanjani ni rafiki na mtu mwenye roho nzuri''.












