Virusi vya corona: Jinsi mafua yanavyoweza kuifurusha corona mwilini

Chanzo cha picha, Getty Images
Virusi vinavyosababisha mafua ya kawaida vinaweza kufurusha virusi vya Covid nje ya seli za mwili, watafiti wanasema.
Baadhi ya vijrusi vinafahamika kushindana ili kuwa ndio vya kwanza katika kusababisha maambukizi,
Na wanasayansi katika Chuo kikuu cha Glasgow wanasema inaonekana virusi vinavyosababisha mafua vinavyofahamika kama rhinovirus humaliza virusi vya corona.
Faida zinaweza kuwa za muda mfupi, lakini virusi vya rhinovirus ambavyo husambaa sana vinaweza bado kusaidia kuzuia makali ya vile vya Covid.
Fikiria kuhusu seli katika pua lako, koo na mapafu, sawa na vyumba vya nyumba.
Wakati virusi vinapoingia ndani, vinaweza kuufungua mlango kwa ajili ya virusi vingine, au vinaweza kuufungua mlango na kuifanya nyumba yake mpya kwa ajili yake pekee.
Virusi vya mafua ni mojawapo ya virusi ambavyo havipendi kukaribisha virusi vingine karibu yake, na karibu kila wakati.
Virusi wengine kama adenoviruses, huonekana kuwa tayari kuwakaribisha virusi wengine katika makazi yake .
'Kuna tetesi kuhusu jinsi virusi vinavyosababisha Covid, vinavyofahamika kama Sars-CoV-2, vinaweza kuishi katika ulimwengu wa ajabu wa "mwingiliano kati ya tofauti ".
Changamoto kwa wanasayansi ni kwamba mwaka wa kutokuwepo kwa utengamano wa kijamii umepunguza kasi ya usambaaji wa virusi vyote na hivyo kufanya utafiti wa muingiliano huu wa virusi kuwa mgumu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kundi la wataalamu katika kituo cha utafiti wa virusi mjini Glasgow nchini Uingereza lilitumia mfano wa utando wa mfumo wetu wa hewa uliotengenezwa kwa aina sawa za seli za utando halisi, na kuuambukiza virusi vya Sars-CoV-2 na vile vya mafua -rhinovirus, ambavyo huwaambukiza zaidi watu, na kusababisha mafua ya kawaida.
Kama rhinovirus na Sars-CoV-2 vingeachiliwa kwa wakati mmoja, rhinovirus pekee ndivyo vingefanikiwa. Kama virusi vya rhinovirus vingeanza saa 24 kabla basi virusi vya corona -Sars-CoV-2 haviwezi kuingia ndani ya seli. Na hata wakati Sars-CoV-2 vilipoingia saa 24 kabla, virusi vya mafua- rhinovirus huvifurusha nje ya seli za mwili.
"Sars-CoV-2 huwa havikimbii, hupewa hifadhi na rhinovirus," Daktari Pablo Murcia aliiambia BBC.
Aliongeza kuwa : "Hii inafurahisha sana kwasababu kama una kiwango kikubwa cha virusi vya mafua rhinovirus,vinaweza kuzuwia maambukizi mapya ya virusi vya Sars-CoV-2 ."
Athari sawa na hii zimewahi kushuhudiwa awali. Mlipuko mkubwa wa rhinovirus huenda ulichelewesha janga la homa ya nguruwe katika baadhi ya maeneo ya Ulaya mwaka 2009.
Vipimo zaidi vilionesha kuwa virusi vya - rhinovirus vilikuwa vinachochea utenda kazi wa mfumo wa kinga ya mwili ndani ya seli, ambao ulizuwia uwezo wa virusi vya corona-Sars-CoV-2 kutengeneza nakala zake.
Wakati wanasayansi walipozuia utenda kazi wa mfumo wa kinga ya mwili, viwango vya virusi vya Covid vilikuwa sawa kana kwamba virusi vya rhinovirus havikuwepo pale .
'Kipindi kigumu cha baridi ' kijacho
Hatahivyo , Covid itaweza kusababisha maambukizi tena pale mafua yatakapokuwa yameisha na mfumo utendaji wa kinga kurejea katika hali ya utulivu.
Dkt Murcia amesema: "Chanjo, pamoja na hatua za usafi, pamoja na muingiliano baina ya virusi vinaweza kushusha matukio ya Sars-CoV-2 kwa kiasi kikubwa, lakini athari ya kiwango cha juu ya kupungua huko itatokana na chanjo ."
Prof Lawrence Young, wa Chuo cha tiba cha Warwick Medical , alisema kuwa virusi vya homa ya mafua vya binadamu vya aina ya rhinoviruses,ambavyo mara kwa mara husababisha mafua ya kawaida "hueambukizwa kwa hali ya juu ".
Aliongeaza kuwa utafiti huu unaonesha "kwamba maambukizi ya mafua haya ya kawaida yanaweza kuathiri Covid-19 na usambaaji wa SarsCoV2, hususan katika miezi ya majira ya kipupwe na baridi msimu ambao mafua huwa ni ya mara kwa mara zaidi ".
Haijafahamika ni vipi hasa mambo yatakavyokuwa katika misimu ya majira ya baridi katika siku zijazo. Virusi vya Corona vina uwezekano wa kuendelea kuwepo, na maambukizi mengine ambayo yamesahaulika wakati wa janga yanaweza kurejea huku kinga dhidi yake ikipungua.
Dkt Susan Hopkins, kutoka Wizara ya afya ya umma ya England tayari ameonya juu ya ''msimu mgumu wa majira ya baridi ''
"Tunaweza kushuhudia ongezeko la mafua.Tunaweza kushuhudia ongezeko la virusi vingine vya mfumo wa kupumua ," alisema.
Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la magonjwa yanayoambukizwa.












