Maandamano Bengal: Wanasiasa wako kwenye shinikizo,watakiwa kurudisha rushwa walizopokea

Chanzo cha picha, AFP
Wakazi wa jimbo la Bengal Magharibi nchini India wameanzisha Kampeni dhidi ya wanasiasa kwa sababu ya kushangaza-wanataka wawakilishi hao warudishe pesa zao walizozipokea kama rushwa kuzirudisha kwa wananchi.
Kiongozi wa jimbo hilo, Mamata Banerjee, amewaambia mawaziri warejeshe rushwa walizozichukua walizopewa na wananchi wakitaka huduma mbalimbali kutoka serikalini.
Makazi ya kiongozi mmoja wa chama chake yalivamiwa na wakazi siku ya Jumatatu, wakitaka warudishiwe fedha zao.
Sasa matukio kama hayo yameripotiwa katika jimbo zima la Bengal.
''Pesa walizochukua....lazima wazirudishe kwa wananchi, tutawafundisha hawa viongozi,'' alisikika mtu mmoja katika maandamano hayo.
Vitendo vya rushwa nchini India si suala geni kwenye siasa za nchini humo, lakini tukio hili halikutarajiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ripoti za maandamano yaliyojitokeza jimboni Bengal hujitokeza kila siku, mwandishi wa habari wa BBC Amitabha Bhattasali anaeleza.
Bi.Benerjee, ni kioongozi maarufu , ambaye aliingia madarakani mwaka 2011.
Lakini kuna dalili kuwa umaarufu wake umeshuka miezi ya hivi karibuni.
Kauli yake hii kuhusu kurejeshwa kwa fedha inaelezwa ni kutaka kurudi tena kwenye safu ya juu kisiasa baada ya kupoteza nafasi ya kiti cha uwaziri mkuu kwa Narendra Modi wa chama tawala cha (BJP).












