Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 21.03.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Tottenham wanajiandaa kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na England, Conor Gallagher, 24, ambaye mkataba wake unamalizika 2025. (Teamtalk).
Liverpool, Tottenham na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vinavyomuhitaji mlinzi wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 26, hata hivyo Fullham wanataka kumpa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City mkataba mpya. (Standard)
Tottenham pia wanavutiwa na winga wa Barcelona na Brazil Raphinha, 27, ambaye mustakabali wake katika klabu hiyo ya La Liga hauko wazi. (Sport)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Liverpool, Arsenal na Chelsea ni miongoni mwa vilabu vinavyohitaji kumnunua beki wa Nottingham Forest raia wa Brazil Murillo, 21. (Mail)
Kiungo wa kati wa Manchester United, Kobbie Mainoo, 18, anakaribia kusaini mkataba mpya na Red Devils. (HITC)
Beki wa Brazil Thiago Silva, 39, anawasiliana na klabu yake ya zamani ya Fluminense huku akitarajiwa kurejea nyumbani, mkataba wake Chelsea utakapokamilika mwishoni mwa msimu kiangazi. (Sun).
Mkufunzi wa Newcastle Eddie Howe, meneja wa zamani wa Chelsea Graham Potter na Gary O'Neil wa Wolves wote wanaweza kuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kibarua cha kuinoa Engaland iwapo Gareth Southgate ataondoka kwenda Manchester United. (Mirror)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Bayern Munich wanaweza kumgeukia Jose Mourinho, ambaye hana kazi baada ya kutimuliwa Roma, kuchukua nafasi ya Thomas Tuchel anayeondoka ikiwa hawataweza kumpata Xabi Alonso anayelengwa. (Mirror)
Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Antonio Conte pia anasakwa na Bayern Munich. (Le Repubblica)
Leeds United iko tayari kumpa kiungo Archie Gray, 18, mkataba ulioboreshwa katika msimu wa joto huku kukiwa na vilabu sita vikubwa vya Ligi Kuu ya Uingereza League vinavyotaka kumnunua. (Football Insider)
Winga wa Benfica na Argentina, Angel di Maria, 36, anafikiria kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Rosario Central . (ESPN)
Mlinzi wa Manchester United, Msweden, Victor Lindelof, 29, anasema hana hamu ya kucheza Saudi Arabia bado, licha ya kuhusishwa na kuhamia ligi ya nchi hiyo msimu wa joto. (Fotbollskanalen)












