Tetesi za soka Ulaya Jumapili 17.07.2022

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic amesisitiza tena msimamo wa klabu hiyo ya Ujerumani kuhusu Cristiano Ronaldo, 37, kwa kukataa uwezekano wa kumnunua mshambuliaji huyo wa Manchester United na Ureno. (SPORT1 via Mail on Sunday)  

Manchester City hawana nia ya kumuuza kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva kwa Barcelona msimu huu wa joto, huku meneja Pep Guardiola bado akimtazama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kama sehemu muhimu ya mipango yake msimu ujao. (Sunday Mirror)

Arsenal wamekubali mkataba wa pauni milioni 30 kumsaini beki wa kushoto wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 25, kutoka Manchester City, huku masharti ya kibinafsi bado hayajakamilika. . (Fabrizio Romano)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea itamnunua beki wa kati wa Sevilla na Ufaransa Jules Kounde, 23, baada ya kushindwa kuafikiana na Manchester City kwa ajili ya kumnunua mlinzi wa Uholanzi Nathan Ake, 27.  (Times - subscription required)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag ameuambia uongozi wa klabu hiyo kuendelea na majaribio yao ya kumsajili kiungo wa kati Mholanzi Frenkie de Jong mwenye umri wa miaka 25 kutoka Barcelona - hata kama hajajiunga nao mwanzoni mwa msimu wao tarehe 7 Agosti.  (Guardian)

Everton wameanza mazungumzo juu ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Uingereza Anthony Gordon, baada ya kukataa ofa ya pauni milioni 35 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kutoka Newcastle United. . (Football Insider)

AC Milan wako kwenye mazungumzo na Tottenham kuhusu kumsajili beki wao Muingereza Japhet Tanganga, 23(Calciomercato in Italian)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wamemtaja De Jong kwenye kikosi chao kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani. (Manchester Evening News)

Juventus wanawasiliana na Atletico Madrid kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 29, ambaye alirejea katika klabu hiyo ya Uhispania msimu wa joto baada ya kumalizika kwa muda wa mkopo wa miaka miwili katika klabu hiyo ya Serie A. (Calciomercato - in Italian)

Paris St-Germain wameungana na Barcelona katika mawindo ya kumsajili kiungo Mwingereza Carney Chukwuemeka kutoka Aston Villa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 aliachwa nje ya kikosi cha meneja Steven Gerrard kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya nchini Australia huku kukiwa na mvutano wa kandarasi. (Sunday People)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Manchester United Muingereza Phil Jones, 30, analengwa na mchezaji mwenzake wa zamani na mkufunzi mpya wa DC United Wayne Rooney. (Daily Star Sunday)

Leeds United wako katika hatua ya juu katika mazungumzo na mshambuliaji wa Uingereza Joe Gelhardt mwenye umri wa miaka 20 kuhusu kuongezwa kwa mkataba. (Football Insider)

Marseille wanajaribu kumsajili beki wa pembeni wa Lens Jonathan Clauss huku Chelsea na Manchester United wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. Atletico Madrid pia wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (90 Min)

Nottingham Forest wametoa pauni milioni 10 kwa Middlesbrough kwa winga Marcus Tavernier, wakati Bournemouth pia wamewasilisha ombi la kumnunua Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 23. (Mail on Sunday)