Tetesi za soka Ulaya Jumatano 16.08.2023

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sofyan Amrabat

Manchester United ipo katika harakati za mwisho kutoa ofa rasmi kwa kiungo wa Fiorentina na Morocco Sofyan Amrabat, 26. (La Nazione - in Italian).

Mchezaji wa kimataifa wa Brazil Alisson Becker hana mpango wa kuondoka Liverpool na ana furaha kuwa kipa namba moja wa meneja Jurgen Klopp. (Anfield Watch)

Timu ya Saudi Arabia Al-Nassr ilisemekana kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 na kwamba Alisson alikuwa na hamu ya kuhamia klabu hiyo. (Footmercato – In French)

Mshambulizi wa Misri Mohamed Salah, 31, ameripotiwa "kuitaka" timu ya Saudi Pro League kufanya mazungumzo na Liverpool kuhusu uwezekano wa uhamisho msimu huu. (Alkass, kupitia Football365)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mohammed Salah

Everton haijapokea ofa kutoka kwa Manchester United kwa kiungo wa Ubelgiji Amadou Onana, 21, na ni ada kubwa tu ya uhamisho itakayomzawadia kuondoka Goodison Park. (Liverpool Echo)

Manchester City wanatazamiwa kuwasilisha ombi jipya la kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na Brazil Lucas Paqueta, 25, katika saa 24 zijazo. (Football Insider)

Crystal Palace wanaamini kuwa Chelsea wamevuka mipaka katika mwenendo wao wakati wa kujaribu kumsajili winga wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Michael Olise, 21. (Mail).

Lazio imeanza mazungumzo na mlinda mlango wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris mwenye umri wa miaka 36 kuhusu uwezekano wa kuhamia Serie A ya Italia (Gianluca di Marzio - kwa Kiitaliano).

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Hugo Lloris

Fulham wamepokea ofa ya karibu pauni milioni 47 kutoka kwa Al-Hilal kwa mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akitaka kuhamia klabu hiyo ya Saudi Arabia. (TalkSport)

Liverpool wanafikiria kuwalenga wachezaji sita wa safu ya kati, akiwemo mchezaji wa Fulham na Ureno Joao Palhinha, 28, na kiungo wa kati wa Crystal Palace na Mali Cheick Doucoure, 23. (Mail).

Mkataba wa West Ham kumsajili beki wa Manchester United na England Harry Maguire umeporomoka kwa sababu wamechoka kumngoja mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kukubali kuondoka kwake Old Trafford. (Guardian)

Kuporomoka kwa mkataba huo kumepunguza uwezekano wa Manchester United kuweza kuweka makubaliano na Bayern Munich kwa beki wa Ufaransa Benjamin Pavard, 27. (Sky Sports)

.
Maelezo ya picha, Benjamin Parvard

Brighton wanavutiwa na beki wa kushoto wa Boca Juniors Valentin Barco huku Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 19 akisemekana kuwa na kipengele cha kumuachia cha takriban £8m. (Brighton Argus)

Kipa wa Uholanzi Tim Krul, 35, anatazamiwa kufanyiwa vipimo vya afya na Luton baada ya makubaliano kufikiwa na Norwich City. (Norwich Evening News)

Manchester City wameratibiwa kupokea 20% ya faida ambayo Southampton inapata kwa mauzo ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19, kwenda Chelsea. (Athletic)