Manchester United: Changamoto za uhamisho zinazomkabili kocha Erik ten Hag msimu huu wa joto

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Erik ten Hag aliiongoza Manchester United kushinda Kombe la Carabao, kutinga fainali ya Kombe la FA na kumaliza nafasi ya tatu kwenye ligi ya Premier katika msimu wake wa kwanza kuinoa.

Mwishoni mwa mkutano wake na wanahabari baada ya Manchester United kushindwa katika fainali ya Kombe la FA mnamo Juni 3, meneja Erik ten Hag aliulizwa kama alikuwa na mipango miwili ya majira ya kiangazi - moja iwapo klabu hiyo ingechukuliwa na mmiliki mpya na iwapo hilo lisengefanyika .

Jibu la Hag lilikuwa la maamuzi.

"Nina mpango mmoja tu ambao ni kuboresha klabu hii na kuboresha timu hii, na ambao nitapigania," alisema. "Nina mawazo yangu lakini pia lazima nifanye kazi na wafanyakazi wangu na wachezaji wangu kufanya vizuri zaidi."

Ninahisi kama ndio njia ya pekee na ya wazi kuiborosha United kutoka kwa United katika kile ambacho kimegeuka na kuwa mateso ya majira ya joto.

Mabadiliko kwa kile kilichokubaliwa kwa ujumla kuwa kikosi ambacho hakiendani na mahitaji kilichowekewa yamekuwa mdogo.

Mason Mount, hatimaye, anatarajiwa kusainiwa baada ya ofa tatu kukataliwa na Chelsea, wakati Zidane Iqbal - ambaye uzoefu wake katika kikosi cha kwanza uliongezwa hadi dakika moja kama akitokea benchi katika mchezo wa kundi la Europa League mnamo Desemba 2021 – ameuzwa kwa timu ya Utrecht ya Uholanzi.

Kando na hayo, Phil Jones na Axel Tuanzebe wameondoka, baada ya mikataba yao imeisha.

Lakini hakuna makubaliano yoyote ya hali ya umiliki. Hakuna suluhu kwa hali ya mkataba wa David de Gea. Na hakuna mchezaji mpya nambari tisa aliyeingia

Angalau inamaanisha kutakuwa na hali ya kuzoeana kwa Ten Hag atakaporejea Carrington kwa ajili ya kuanza kwa mazoezi ya kabla ya msimu wiki ijayo.

Lakini, kutokana na shughuli katika klabu pinzani, Mholanzi huyo anakabiliwa na wiki chache ngumu.

Hali tata ya umiliki wa klabu hiyo

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wamiliki wa United, familia ya Glazer kwanza walisema walikuwa wanafikiria kuuza klabu hiyo mnamo Novemba
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Takriban mashabiki 30 pekee ndio waliokuwa Old Trafford mnamo tarehe 27 mwezi Juni kwa maandamano ya hivi punde ya kundi la 1958 ambalo linafanya kampeni ya kukomesha umiliki wa familia ya Glazer wa klabu hiyo.

Kwa haki, idadi hiyo labda iliathiriwa na ukweli kwamba hakuna mtu aliyetarajia tathmini ya "mbadala wa kimkakati" kwa United kuendelea siku 231 (hadi 30 Juni) baada ya kuzinduliwa.

Vyanzo vimeelezea mchakato huo kama "mgumu" na vilisema mikataba inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuliko ile ya United kufutiliwa mbali.

Hii inaweza kuwa kweli, lakini ni mara chache sana wanaweza kufanya hivyo huku kukiwa na utangazaji mwingi na mijadala.

Kwa watu wa nje inaonekana United wamekwama, na hadi iamuliwe nani anaiongoza klabu kwa muda mrefu, mbinu na mwelekeo vinakosekana.

Mtazamo huu sio wa haki kwa wale ambao wako Old Trafford, wakijaribu kutekeleza kile wanachoamini kuwa ni maamuzi sahihi.

Lakini kukosekana kwa utulivu kileleni huathiri shirika lolote, na katika mazingira ya kutosamehe kama vile Ligi ya Premia, kuwapa wapinzani faida kunaweza kuonekana tu kuwa hasi.

Mshambuliaji nambari tisa mgongoni

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harry Kane aliifungia England mabao mawili dhidi ya Macedonia Kaskazini kwenye Uwanja wa Old Trafford mwezi Juni

Imekuwa dhahiri kwa muda mrefu kazi kubwa ya Ten Hag msimu wa joto ilikuwa kutafuta mshambuliaji wa kati.

Harry Kane ndiye chaguo la kwanza la wazi, lakini sauti za awali zilipendekeza kumvutia nahodha wa Uingereza kutoka Tottenham haingewezekana kwa bei ambayo United wangeweza kumudu.

Badala yake, Ten Hag anawatazama vijane wadogo.

Rasmus Hojlund wa Atalanta amekuwa akitajwa mara kwa mara na fowadi huyo wa Denmark mwenye umri wa miaka 20 tayari ana hat-trick katika mechi ya kimataifa katika jina lake.

Randal Kolo Muani pia yuko kwenye rada za United, ingawa mshambuliaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 anachukuliwa kuwa mchezaji wa kiwango cha juu na Eintracht Frankfurt na ada ya uhamisho inayohitajika kumnunua inaweza kuwa kizuizi.

United wana chaguo la kumtumia Marcus Rashford katika nafasi ya kati, ingawa haipendi, wakati Anthony Martial bado ana mwaka mmoja kwenye mkataba wa miaka mitano na nusu aliosaini Januari 2019.

Masuala ya kipa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kipa David de Gea wa Manchester United baada ya kushindwa katika fainali ya Kombe la FA mwezi Juni

Hata iwapo hakuna uhakika kuhusu mustakabali wa kipa De Gea kusalia United, Ten Hag lazima atazame mbele zaidi.

Kiwango cha Andre Onana kwa Inter Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City kilikuwa kielelezo cha kile kipa wa kisasa anatarajiwa kuzalisha akiwa na mpira miguuni mwake.

De Gea hawezi kufikia kiwango sawa kwa msingi thabiti, na hadi dosari hiyo kwenye kikosi cha Ten Hag itakapotatuliwa ni vigumu kuona jinsi timu yake inavyoweza kutoa kiwango kinachotakiwa na Mholanzi huyo.

Ni sawa kudhani Dean Henderson anaamini kuwa anaweza kufanya kile ambacho Ten Hag anadai.

Swali kubwa ni iwapo Ten Hag ana mtazamo sawa na mchezaji ambaye alisema wazi kuwa anataka kuondoka Old Trafford kabla ya kuwasili kwa bosi huyo wa zamani wa Ajax majira ya joto ili kumzuia kupata fursa ya kumshawishi Henderson kubaki.

Je, United wanaweza kuuza vizuri?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Je, hatma ya Scott McTominay (kushoto), Anthony Elanga (katikati) na Fred (kulia) ni ipi Manchester United?

Mbali na mifano ya mara kwa mara ya Manchester United kushindwa kununua wachezaji wazuri, kuna thibitisho pia kwamba pia hawawezi kufanya biahara nzuri na wachezaji inaotaka waondoke.

Ikizingatiwa wanahitaji kujipata fedha katika soko la uhamisho ili kuimarisha bajeti ya uhamisho ya Ten Hag, kuna ongezeko la uchunguzi unaoelekezwa kwa kile ambacho mkurugenzi wa kandanda ya biashara John Murtough anaweza kufanya.

Hatima ya wachezaji 12 wakuu iko wazi kujadiliwa.

Sio wote watakaoondoka, na ikiwezekana baadhi ya wale wanaofanya hivyo hawatavutia zabuni kubwa.

Wachezaji kama vile Brandon Williams, Eric Bailly, Alex Telles, Anthony Elanga na Donny van de Beek wanaweza kuwa wanataka kuondoka, Fred na Scott McTominay wanalazimika kutathmini hatma yao kwa kuzingatia ujio wa Mount, huku Dean Henderson na Hannibal Mejbri wakivutia klabu kadhaa baada ya kucheza kwa mkopo .

Hata hivyo, kwa upande wa Harry Maguire, Jadon Sancho na Anthony Martial, kuna kukubali hasara ya ada kubwa ya uhamisho, wakijua kuwa wako kwenye mikataba ambayo huenda isilinganishwe mahali popote mbali na kwamba wanahitaji kubadilishwa.

Hii ina uwezo wa kusababisha tatizo la kifedha ambalo linaweza kufanya kuondoka kutowezekana.

Walakini, katika ulimwengu mzuri, Murtough ataunda mazingira ya kutosha kumruhusu Ten Hag kupata wachezaji anaowataka.

Chini ya Louis van Gaal, Jose Mourinho na Ole Gunnar Solskjaer, United ilipiga hatua kubwa katika msimu mmoja, lakini ikarudi nyuma hadi sasa hivi.

Kutokana na kuongezeka kwa ushindani unaowakabili, hawawezi kumudu kurudia makosa yaliyopita.