Malkia wa Sheba:Kwa nini wanawake wa nchi hizi wanajihusisha na mwanamke anayetajwa katika Biblia na Quran?

Chanzo cha picha, Getty Images
"Mimi ni kizazi cha Malkia wa Sheba."
Kauli moja inayosemwa leo na wanawake kutoka Yemen, Ethiopia na Somalia inaelezea zaidi ya hadithi ya mtu anayepatikana na katika Biblia na Koran.
Imejaa utu na ni kinyume na masaibu yote, lakini pia imejaa, historia ya miaka ya nyuma ya utawala wa mauaji na chuki za enzi za mababu.
Mwandishi wa Colombia Laura Restrepo amejikita katika riwaya yake ya " Song of ancient lovers" katika Malkia wa Sheeba, Queen of Sheba, kiumbe cha ajabu au chimera, ambacho kiliteswa kuanzia enzi za Thomas Aquinas hadi André Malraux au Gérard de Nerval na kukifananisha na maafa ya kibinadamu katika Ghuba ya Aden, inayotenganisha Upembe wa Afrika na Rasi ya Arabia. Mahali ambapo panapatikana hali halisi na hadithi ya Malkia wa Sheba kwa pamoja.
Akizungumzia kuhusu Bos Mutas wa jinsia ya kiume, ambaye anakwenda kumtafuta malkia wa kufikirika , mwandishi Restrepo anakumbuka kile alichokutana nacho wakati wa safari yake alipoambatana na madaktari wa shirika lisilo la kiserikali la Madaktari wasio na mpaka ( Doctors Without Borders), miaka saba iliyopita, ambapo alikuwa katika nchi za Yemen, Ethiopia na katika mpaka na Somalia.
Kwa kiasi fulani ilikuwa tu kwa bahati. Safari hii ilianza kwa mwaliko kutoka kwa Madaktari wasio na mpaka. Waliwapigia simu waandishi wa habari ili wawapeleke katika mizozo ambako mizozo ya kibinadamu imekithiri kiasi kwamba vyombo vya habari hata havijali kuifuatilia tena.
Sikujua mengi kuhusu Yemen, ninakiri, anasema, isipokuwa kujua kuwa ilikuwa ndani ya Ulimwengu wa Kiarabu.
Kumbukumbu pekee niliyokuwanayo ilikuwa ni Malkia wa Sheba-(Queen of Sheba), hadithi niliyoisoma katika kitabu kizuri sana kidogo ambacho nilikuwa nimekisoma kilichioandikwa na André Malraux, ambaye alikuwa akimtafuta kwenye ndege katika miaka ya 1940.
Unapofika katika Upembe wa Afrika unajipata katika maafa makubwa ambayo yanawakumba wanawake na watoto, wahamiaji wengi wanaotoka katika eneo lote la upembe wa Afrika. Maelfu kwa maelfu ya wanawake kutoka Kenya, Ethiopia, Eritrea wanaotafuta maeneo maisha katika eneo ambako maisha hayawezekani.
Mwandishi André Malraux alikwenda pale kumtafuta Malkia wa Sheba katika magofu ya kasri zake na hakumpata.
‘’Na sasa ninampata katika kila mmoja wa wanawake hawa ambao wanatembea miguu peku, wakichomwa na jua na chumvi, wakivuka jangwa kutafuta maisha ambayo hayapo’’, anasema.

Chanzo cha picha, EDITORIAL ALFAGUARA
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Ni jinsi gani riwaya hii inayohusisha mkasa wa Yemen, Somalia na Ethiopia na wa Malkia wa Sheba ilizaliwa?
Kwa kiasi fulani ilikuwa ni kwa bahati . ilianza na mwaliko kutoka kwa shirika la Madaktari wasio na mpaka (Doctors Without Borders). Waliwaalika waandishi wa habari kuwachukua katika mizozo ambako mizozo ya kibinadamu imesahaulika kiasi kwamba vyombo vya habari haviiangazii tena .
Hadi wakati ule, Malkia wa Sheba hakuhusika na vipuli vya fedha, ngamia weupe, nguo za hariri ambazo nchi za Magharibi zimekuwa zikimvalisha.
Lakini, la kushangaza bado ni kwamba wanawake wa hawa wenye masibu tele walipoulizwa na mwandishi, inashangaza kwamba kwamba wengi wao pia walijibu kwa kujigamba na kiburi : "Mimi ni kizazi cha Malkia wa Sheba." Ni sawa na kusema: "Wewe ni nani? Unaniona kama omba omba, lakini ninatoka katika ukoo wa mababu waliokua matajiri ambao wataendelea kuishi hata wakati utamaduni wako utakapokuwa umesahaulika ."
Wanasema wazi na kwa kukufahamisha kwamba huo ndio utambulisho wao, wa kunusurika. Iliniumiza na ikanifanya nifikirie kwamba , "hii sio ardhi ya maafa, ardhi hii ni urithi wa utamaduni, iliyojaa ushairi na hadithi unaofanana licha ya maafa wanayopitia wenyeji ."

Chanzo cha picha, Getty Images
Malkia wa Sheba haikuwa hadithi ambayo ningeitambua isipokuwa kupitia kitabu kidogo cha Malraux, ambacho ni kizuri sana, kwasababu Malraux hampati katika eneo halisi, lakini anampata katika kitabu chake.
Katika kuangalia na kufanya utafiti katika utamaduni wa Kiarabu na pia katika utamaduni wa Magharibi kutaka kumjua Malkia wa Sheba, inashangaza kwamba mwanamke pekee ambaye anaonekana katika wakati ule katika ushuhuda wa ajabu kama Biblia haelezewi hivyo kama mtakatifu, au kahaba , au kwasababu alikata nywele za mtu, au kwasababu alikuwa mmoja wa mashahidi wa kiimani, ila kwasababu alikuwa ni mwanamke mwenye hekima na mwenye mamlaka.
Hekima, aliyependa ujuzi…ndio mambo yanayomuelezea na mambo hayo yalifanana maswali yale niliyoyadadisi , ambayo ni kwamba wanawake ambao waliniambia kuwa hawana chochote hawana nyumba, chakula , wagonjwa, nilipowauliza, "ni nini mnatafuta?, mnataka nini?", walisema: "ninataka kujielimisha, ninataka kuwa mwalimu, au ninataka kuwa muuguzi au ninataka kuwa daktari ."anasema mwandishi.
Hadithi hii ya Malkia wa Sheba inamaana gani kwa wanawake ?
Kwanza, unakua na alama ya ukuu. ‘’Sina lolote, lakini mimi ni kizazi cha Malkia wa Sheba’’, walituambia.
Wanawake hawa wengi wao wanaishi ufukweni mwa bahari kweney ghuba ya Aden, ndani ya makambi ya wakimbizi.

Kwa upande mwingine, nilikua katika timu ya madaktari wasio na mpaka. Nilikua na vijana wadogo kutoka maeneo mbali mbali ya dunia, kutoka Somalia kwenyewe, Kutoka Yemen, ambao walikuwa wakijaribu kutoa msaada.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika kitabu chake mwandishi anaangazia pia masaibu, ya wanawake wa Yemen, Ethiopia na Somalia
Mizozo ya ndani baina ya makundi tofauti ya kijamii na wakati huo huo , vita hivi haiwezekani kuvishinda. Kwa sababu hii, tukirejea tena katika kauli "Mimi ni kizazi cha Malkia wa Sheba ", kwamba majivuno pia ni njia ya kuelezea ya utashi wa kupambana. "Wanataka kunifuta katika sayari, lakini sio kweli kwamba ni mtu asye na thamani. Mimi ni mtu wa maana na ninapambana."

Chanzo cha picha, JUAN CARLOS THOMAS
Katika safari zake na Madaktari wasio na mpaka, mwandishi alitembelea Yemen, Ethiopia na mpaka wa Somali.
Katika kitabu chake mwandishi anazungumzia kuhusu ukeketaji, ambao bado wanawake wanalazimishwa kuufanya katika nchi nyingi.
Mwandishi anasema ni kitendo cha ukatili.
Pia ni jambo muhimu kuiangalia dunia kupitia macho ya Madaktari wasio na mpaka, na mtanziko unaowakabili.
Kwa upande mwingine, wanawasili katika nchi wakiwa na wajibu na uamuzi wa kuheshimu mila za nchi hiyo.
Lakini wakayti huo huo wanakutana na vitu vya utisha, kama vile kuenea kwa utamaduni na mila ya ukeketaji wa wanawake, ambao unafanyika katika eneo lote hilo.
Je unawezaje kuheshimu utamaduni wa nchi wakati mwanamke aliyeathiriwa anafika kukwambia , tafadhali nifungue na unitibu maambukizi ambayo yamenifanya niumie katika maisha yangu yote ? Maelfu ya wanawake hufa kutokana na ukeketaji.
Kufungwa kwa sehemu ya uke kunaweza kuharibu kisimi au kuziba sehemu yake. Mara nyingi huwa kinafungwa sana kiasi kwamba ni matone matatu tu ya damu ya mwezi yanaweza kutoka wakati wa hedhi.
Hali hii huwafanya wanawake kuumia na kutengwa na jamii zao.
Ni ukatiki, anasema. Huwafanya wanawake waoze ndani ya uke wao, inawafanya wakataliwe.
Madaktari wana njia zao za kumsaidia kila mwanamke anayekuja katika hali hizi, lakini bila shaka ni hali ngumu kwasababu ya uwepo mkubwa wa Taliban.















