Mji wa chini ya ardhi wa Uturuki wa watu 20,000

RalucaHotupan/Getty Images

Chanzo cha picha, RalucaHotupan/Getty Images

 Misukosuko mikali ilipeperusha mchanga hewani nilipokuwa nikitembea katika Bonde la Upendo la Kapadokia. Milima yenye rangi ya waridi na manjano ilipendezesha mandhari yenye makovu ya rangi nyekundu, na miamba mikubwa  ilionekana kwa mbali.

Kulikuwa na ukame, joto, upepo lakini madhari ilikua ya kuvutia.

Miaka 1000 iliyopita, mazingira haya tete, ya volkeno kwa kawaida yalichonga miiba inayonizunguka katika umbo lake lenye muonekano wa uyoga, ambalo sasa linavutia mamilioni ya wageni kufika katika eneo hili nchini Uturuki.

Lakini katika eneo hili, maajabu ya uwiano sawa yalifichwa kwa karne nyingi; jiji la chini ya ardhi ambalo lingeweza kuficha mahali wanapokaa Zaidi ya watu 20,000 kwa miezi kadhaa kwa wakati mmoja.

Mji wa kale wa Elengubu, unaojulikana leo kama Derinkuyu, umechimbwa zaidi ya mita 85 chini ya uso wa Dunia, ukiwa na Zaidi ya vichuguu 18, Ukiwa ndio mji mkubwa zaidi uliochimbwa chini ya ardhi duniani, ulikuwa ukitumika karibu mara kwa mara kwa maelfu ya miaka, wakati Fulani ukiwa chini ya utawala wa Wafrigi hadi Waajemi na kisha Wakristo wa Enzi ya Byzantine.

Hata hivyo mji huu ulitelekezwa katika miaka ya 1920 na Wagiriki wa Kapadokia walipokabiliwa na kushindwa wakati wa vita vya Ugiriki na Uturuki na kukimbilia Ugiriki.

Sio tu kwamba vyumba vyake vinavyofanana na mapango, lakini pia vimesambaa kwenye eneo kubwa, huku ikidhaniwa kuwa kuna Zaidi ya miji 200 midogo midogo, tofauti ya chini ya ardhi ambayo pia imegunduliwa katika eneo hilo inaweza kuunganishwa kwenye vichuguu hivi, na kuunda mtandao mkubwa wa chini ya ardhi.

Kulingana na mwongozaji wangu, Suleman, Derinkuyu "iligunduliwa tena" mwaka 1963 na mwenyeji asiyejulikana baada ya kupoteza kuku wake.

Alipokuwa akikarabati nyumba yake, kuku hao walitoroka kupitia mwanya mdogo uliopatikana wakati wa ukarabati huo ambao hawakuonekana tena.

Baada ya uchunguzi wa kina na kuchimba chini kidogo, Mturuki huyo aligundua njia ambayo ilikua na giza. Ilikua njia ya kwanza kati ya zaidi njia 600 zilizoopatikana ndani ya nyumba za kibinafsi zinazoelekea kwenye jiji la chini ya ardhi la Derinkuyu.

RalucaHotupan/Getty Images

Chanzo cha picha, RalucaHotupan/Getty Images

Maelezo ya picha, Derinkuyu ina viwango 18 vya mahandaki yenye mashimo ya mita 85kwenda chini
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tarehe halisi ya ujenzi wa eneo hilo bado haijafahamika, lakini  baadhi wanasema huenda ikawa ni mwaka 370 BCE, ndiyo kazi ya zamani zaidi iliyoandikwa ambayo inaonekana kuandikishwa katika historia.

Katika kitabu hicho, anataja watu wa Anatolia, ndani au karibu na eneo la Kapadokia, wanaoishi chini ya ardhi katika nyumba zilizochimbwa badala ya makazi maarufu ya mapangoni ambayo yanajulikana sana katika eneo hilo.

Kulingana na Andrea DeGiorgi, profesa mshiriki wa masomo ya kitamaduni katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Florida, Kapadokia inafaa kipekee kwa aina hii ya ujenzi wa chini ya ardhi kwa sababu ya ukosefu wa maji kwenye udongo na mwamba wake unaoweza kunyumbulika kwa urahisi. "Jiomofolojia ya eneo hili inafaa kwa uchimbaji wa maeneo ya chini ya ardhi," alisema, akifafanua udongo wa chokaa, ingekuwa rahisi kuchonga kwa zana rahisi kama vile majembe na panga.

 Hata hivyo, inaelekea kwamba sehemu kubwa ya jiji hilo ilijengwa na wasanifu majengo wenye ujuzi wa hali ya juu wakati wa zama za chuma ambao walikuwa na uwezo wa kujenga majengo marefu ya chini ya ardhi.

"Wafrigi walikuwa mojawapo ya himaya za awali za Anatolia," alielezea DeGiorgi. Ingawa ni vigumu, ufalme wao ulienea kujumuisha sehemu kubwa ya Anatolia ya Magharibi na kati, kutia ndani eneo la Derinkuyu."

RalucaHotupan/Getty Images

Chanzo cha picha, RalucaHotupan/Getty Images

Hapo awali, huenda Derinkuyu ilitumiwa kuhifadhi bidhaa mbalimbali, lakini kusudi lake kuu lilikuwa kama kimbilio la muda kutoka kwa wavamizi wa kigeni, huku Kapadokia ikiona msururu wa mara kwa mara wa milki kuu katika karne zote. "Mfululizo wa himaya na athari zake katika mandhari ya Anatolia inaelezea kukimbilia kwa makazi ya chini ya ardhi kama Derinkuyu," DeGiorgi alielezea. "Ilikuwa wakati wa uvamizi wa Kiislamu wa Karne ya 7 [kwenye Milki ya Byzantine yenye Wakristo wengi, hata hivyo, makazi haya yalitumiwa kikamilifu." Wakati Wafrigi, Waajemi na Waseljuk, miongoni mwa wengine, wote waliishi eneo hilo na kupanua mji wa chini ya ardhi katika karne zilizofuata, idadi ya watu wa Derinkuyu iliongezeka hadi kwa wingi wakati wa Enzi ya Byzantine, na karibu wakaazi 20,000 waliishi chini ya ardhi hiyo.

Leo hii, unaweza kupata hali halisi yae neo hili kwa kulitembelea kwa kulipa kiasi cha lira 60 tu za Kituruki (£2.80).

Nilipokuwa nikishuka kwenye vichuguu vilivyo na uchafu na vyembamba, kuta zikiwa  zimeanza kubomoka kutokana na kudumu kwa muda mrefu  nilihisi uwezo wa hali ya juu uliotumika kwa miaka hiyo kabla hata teknolojia haijakua kama leo hii.

Ukiwa na mwanga hafifu kwa mwanga wa taa, miamba ya duara ya nusu tani iliziba milango kati ya kila ngazi 18 na ilikuwa ya kusogezwa tu kutoka ndani. Mashimo madogo ya duara katikati ya milango hii mirefu yangeruhusu wakazi kuwarushia wavamizi mikuki huku wakiliweka eneo lao salama.

Kila ngazi ya mji huu ilitengenezwa kwa uangalifu kwa matumizi maalum. Mifugo iliwekwa kwenye mazizi karibu na mlangoni ili kupunguza harufu na gesi zenye sumu zinazozalishwa na ng'ombe, na pia kupunguza.

Tabaka za ndani za jiji zilikuwa na makazi, sehemu za mapishi, shule na nafasi za mikutano.

Derinkuyu ilikuwa na malango, zaidi 600 katika nyumba za kibinafsi

Chanzo cha picha, RalucaHotupan/Getty Images

Maelezo ya picha, Derinkuyu ilikuwa na malango, zaidi 600 katika nyumba za kibinafsi

Lakini cha kustaajabisha zaidi ni mfumo tata wa uingizaji hewa na ulinzi mzuri ambao ungetoa kwa jiji zima hewa safi na maji safi. Kwa kweli, inadhaniwa kuwa ujenzi huu wa zamani wa Derinkuyu ulizingatia vipengele hivi viwili muhimu.

Zaidi ya mashimo 50 ya uingizaji hewa, ambayo yaliruhusu mtiririko wa hewa ya asili kati ya makao mengi ya jiji na barabara za ukumbi, zilisambazwa katika jiji lote ili kuzuia shambulio linaloweza kusababisha kifo kwenye usambazaji wao wa hewa.

 Ingawa ujenzi wa Derinkuyu ulikuwa mzuri sana, sio mji pekee wa chini ya ardhi huko Kapadokia.

Ukiwa na kilomita za mraba 445, ni mji mkubwa zaidi kati ya 200 iwapo utahesabu miji ya chini ya ardhi chini ya uwanda wa Anatolia.

Pia kuna mioundombinu ya vifaa vya dhadhura ili kusaidia iwapo kungetokea tatizo lolote.

Lakini siri za chini ya ardhi za Kapadokia bado hazijajulikana zote. Mnamo mwaka  2014, jiji jipya na ambalo linaweza kuwa kubwa zaidi la chini ya ardhi liligunduliwa chini ya eneo la Nevsehir.

Historia ya uwepo wa watu katika eneo hili la Derinkuyu ilifikia mwisho mwaka 1923 wakati Wagiriki wa Kapadokia walipohama.

Zaidi ya miaka 2,000 baada ya uwezekano wa kuundwa kwa jiji hilo, Derinkuyu ilitelekezwa kabisa.

Uwepo wake ulikuwa umesahaulika kwa dunia ya kisasa mpaka pale kuku waliokosea njia walipoingia katika eneo hilo na kuanza kutafuwa na mmliki wao, huu ukawa mwanzo wa kufahamika kwake tena na kuwa miongoni mwa vivutio vikubwa vya utalii nchini Uturuki.