Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Mustakabali wa Bruno Fernandes Man United utategemea kufuzu katika klabu bingwa

.

Chanzo cha picha, GETTY

Maelezo ya picha, Bruno Fernandes
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United iko tayari kumpa kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes mkataba ulioboreshwa wenye thamani ya hadi £400,000 kwa wiki - lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 atatoa uamuzi kuhusu mustakabali wake Old Trafford ikiwa klabu hiyo itafuzu kwa Ligi ya Mabingwa. (Mirror)

Beki wa Tottenham Micky van de Ven, 24, anasakwa na Barcelona, ​​ambao wanatazamiwa kuzidisha juhudi zao za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi msimu wa joto. (Sport - Spanish)

Mustakabali wa muda mrefu wa kiungo wa kati wa Uingereza Kobbie Mainoo katika klabu ya Manchester United bado uko hewani huku mazungumzo ya kumpa mkataba mpya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 yakiendelea. (Mail - Subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Micky van da Ven

Arsenal wameambiwa na Inter Milan kwamba mshambuliaji wa Kiitaliano mwenye umri wa miaka 20 Pio Esposito hauzwi kwa bei yoyote. (Gazzetta dello Sport - In Italy)

Juventus wako tayari kufufua nia yao ya kumnunua fowadi wa Paris St-Germain Mfaransa Randal Kolo Muani, 27, ambaye kwa sasa yuko Tottenham kwa mkopo. (Calciomercato - In Italy)

Aston Villa ni moja wapo ya vilabu vinavyovutiwa na kiungo mshambuliaji wa Wales Harry Wilson, 28, ambaye mkataba wake na Fulham unamalizika msimu wa joto. (Fabrizio Romano)

Brentford wanatazamiwa kuwatoa hadi wachezaji watano msimu wa joto, akiwemo kiungo wa kati wa Ureno, Fabio Carvalho, 23. (The I Subscription Required)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Carvalho

Manchester United hawana nia ya kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 27, msimu wa joto licha ya kutakiwa Aston Villa na Fulham. (Football Insider)

Juventus wanaonekana kuwa wamepiga hatua katika kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 26, ambaye mkataba wake unakamilika msimu wa joto. (Tuttosport - In Italy)

Kiungo wa kati wa Bayern Munich na Austria Konrad Laimer, 28, wamesitisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya kwani kuna pengo kubwa kati ya matarajio ya pande zote mbili. (Sky Sports in Germany)