Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 07.02.2024

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Kiungo wa kati wa Argentina, Enzo Fernandez, 23, anafikiria kuondoka Chelsea mwaka mmoja tu baada ya kujiunga na klabu hiyo kwa euro milioni 121 kwa kandarasi ya miaka minane na nusu. (FootballTransfers.com)
Wachezaji wa Chelsea wamelalamika kuwa mbinu za ufundishaji za Mauricio Pochettino na wafanyakazi wake ni finyu, huku wachezaji wapya waliowasili wameonyesha majuto juu ya mikataba yao ya muda mrefu. (Athletic)
Hata hivyo, Chelsea itasubiri hadi mwisho wa msimu ili kutathmini mustakabali wa Pochettino kama meneja. (Football.London)
Liverpool wamefanya mawasiliano na meneja wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso kufuatia uamuzi wa Jurgen Klopp kuwa ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu. (Footmercato)

Chanzo cha picha, Getty Imagges
Manchester United wanataka kuwekeza zaidi kusajili vijana wakati wa majira ya joto, huku mshambuliaji wa Crystal Palace mwenye umri wa miaka 22 kutoka Ufaransa, Michael Olise na mlinzi wa Everton mwenye umri wa miaka 21 Mwingereza, Jarrad Branthwaite wanalengwa kusajiliwa. (inews)
Manchester City bado haijamsajili winga wa Brazil Savio, 19, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Girona ya Uhispania kutoka Troyes ya Ufaransa, lakini mazungumzo yamefanyika na timu hiyo ina matumaini ya kumsajili. (ESPN)
Crystal Palace wanafikiria mustakabali wa Roy Hodgson kama meneja - lakini klabu hiyo inatatizika kupata mbadala wake. (Times)

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES
Mshambulizi wa Manchester United, Muingereza, Mason Greenwood, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Getafe, yuko kwenye orodha ya Atletico Madrid ya washambuliaji ambao wanafikiriwa kusajiliwa msimu wa joto. (Telegraph)
United italenga wachezaji ambao wanaingia mwaka wa mwisho wa kandarasi zao msimu huu wa joto na wanaweza kuzungumza na mchezaji kama vile kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Joshua Kimmich, 28, mshambuliaji wa Lille ya Canada, Jonathan David, 24, na kiungo wa kati wa Nice, Mfaransa, Khephren Thuram, 22. (ESPN )
Liverpool wanamfuatilia mshambuliaji wa Juventus na Italia, Federico Chiesa, 26. (HITC)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambulizi wa Norway, Erling Haaland, 23, hana mpango wa kuondoka Manchester City huku kukiwa na uvumi kuwa anaweza kujiunga na Real Madrid . (Football Insider)
Arsenal wanataka kumbakisha winga wao wa chini ya miaka 19 wa England, Amario Cozier-Duberry, 18, huku Newcastle, Ajax, Borussia Dortmund, Wolves na Anderlecht wote wakimtaka. (Fabrizio Romano)
Manchester United inamfuatilia winga wa kimataifa wa Copenhagen na Sweden, Roony Bardghji, 18. (Sun)
United hawana mpango wa kumpa kiungo wa Ureno, Bruno Fernandes, 29, nyongeza ya mshahara licha ya nia ya kutaka kusajiliwa Saudi Arabia. (Football Insider)
Imetafsiriwa na Rashid Abdallah












