'Warusi walipovamia mji wangu wa Kherson niliamua kurekodi kilichotokea'

Chanzo cha picha, Dmytro Bahnenko
Wakati Urusi ikihangaika kuwahamisha raia wake kutoka mji wa Kherson kwa kutarajia mashambulizi ya jeshi la Ukraine, Dmytro Bahnenko, raia wa Ukraine, anatafakari juu ya miezi ambayo yeye na wapendwa wake waliishi chini ya uvamizi wa Urusi, ambayo aliirekodi kwa siri.
kipindi cha BBC Eye. Mstari "Nimeona roboti leo," binti yangu Ksusha mwenye umri wa miaka mitano alininong'oneza huku nikimrekodi chini ya meza.
"Ilikuwa inaruka ... ilitaka kuniua." Haikuwa wazi ni nini Ksusha aliona - au hakuona - siku hiyo ili kuchochea picha hiyo ya kutatanisha. Lakini ni wazi alikuwa amechanganyikiwa.
Kila kitu kimebadilika tangu wanajeshi wa Urusi walipooita mbele ya dirisha la nyumba yetu mchana wa Machi mosi na nilianza kurekodi hali ya maisha yetu kwa ajili ya kipindi cha uchunguzi cha BBC Eye.
Katika kazi yangu ya uandishi wa habari wa nchini sikuwahi kufikiria nitarekodi filamu ya uvamizi wa mji wetu - makao makuu pekee ya kikanda nchini Ukraine yaliyotekwa na Warusi.
Kinaya ni kwamba kwa miongo kadhaa, Ukraine ilisaidia kulisha ulimwengu, lakini katika siku hizo za mapema tulikuwa na shida kupata bidhaa za kimsingi. "Nilifanikiwa kupata viazi vya mwisho," mwanamume aliyechoka aliniambia nilipiga picha katikati mwa jiji mapema Machi. Ilikuwa bado saa tisa asubuhi.
Lakini watu wa Kherson hawakuwa tayari kujiuzulu kwa hatima yao.
Maandamano ya kupinga uvamizi huo yalianza tangu mwanzo na yalizidi kuwa makali kadri wiki zilivyozidi kwenda.
Wanajeshi wa Urusi walionekana kushangaa - katika akili zao walikuwa wamefika kama "wakombozi".
Nilianza kwenda kwenye kanisa la Othodoksi kwa baiskeli, ambako jumuiya ya mahali hapo ilikusanyika na huko ningeweza kuwasaidia wengine kufanya kazi zinazofaa. Nilikutana na kuhani mwenye haiba, Baba Serhiy Chudynovych.

Chanzo cha picha, Dmytro Bahnenko
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Alikuwa na nguvu fulani, akijihusisha na mradi mmoja hadi mwingine.
Alikuwa msimamizi wa kituo cha jamii, mkahawa na mfanyakazi wa nywele anayesafiri na, labda muhimu zaidi, alikuwa akihatarisha maisha yake akivuka safu za kijeshi ili kukusanya dawa ambazo hazikuwa zikipatikana tena huko Kherson.
"Inatia hofu wakati unaendesha gari na unapigwa risasi - lazima uondoke haraka," aliniambia Mdundo huo wa utulivu wa kiasi, ulioangaziwa na wakati wa hatari kubwa, uliashiria mdundo wa maisha yetu.
Na hata nyakati hizo za utulivu zilianza polepole kuwa za wasiwasi.
Katika mji mzima, wiki mbili baada ya maandamano ya kwanza ya wanajeshi wa Urusi kuelekea Kherson, Padre Serhiy alichukua uamuzi wa kusimamia mazishi ya hadharani ya mwanajeshi wa Kiukreni aliyefariki, na kuitangaza moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii kwa wale ambao hawakuweza kuhudhuria. Haikuwa hatari bure.
Padre Serhiy alikiri kwamba kutoa hesima za mwisho kwa mwanajeshi wa Ukraine aliyekufa kunaweza kutafsiriwa kama uchochezi wa jeshi la Urusi.
Wakati huo huo, maandamano dhidi ya uvamizi huo yaliendelea, na mnamo Machi 21, hali ilibadilika.
Jeshi la Urusi lilianza kurusha mabomu ya machozi na kurusha mabomu ya kushtukiza. Watu wengi walijeruhiwa.
Hii ilifuatiwa na hatua kali zaidi. Watu zaidi na zaidi walitoweka miongoni mwao wanaharakati, wale walio na uhusiano na mamlaka za Ukraine, pamoja na waandishi wa habari. Baadhi ya watu walikamatwa wakati wa maandamano hayo, wengine majumbani mwao.
Wengine waliachiliwa, wengine hawakurudi tena. Niliogopa kwamba ningefuata.
Je, itachukua muda gani kabla ya jumbe zangu kupatikana kwenye simu ya mmoja wa wafungwa? Au, kusimamishwa na kupekuliwa na video zangu kupatikana?

Usiku uliofuata, tulikutana na dada yangu mjamzito Maryna na mume wake Vitaly kwenye nyumba ambayo mimi na wazazi wetu tuliishi pamoja tulipokuwa tukikua.
Huko - kwenye meza ya jikoni ambapo tulipata kifungua kinywa tukiwa watoto - tulijadili vita. Maryna alikuwa akiangalia bei za madereva zinazotozwa ili kuwatoa watu nje ya mji.
Walianza kwa $1,500 ili tu kuvuka mstari wa mbele na kufanya umbali mfupi hadi Mykolaiv. Haiwezekani kulipa, lakini walianza kuhisi kukata tamaa, Maryna hakutaka kuzaa wakati wa kazi hiyo.
Lich aya hayo, haikuwa salama tena kwa Vitaly kwenda kazini. Aliendesha jumba la kifahari la kibinafsi - hoteli, stables, hifadhi ndogo ya wanyama - nje kidogo ya jiji, ambayo ilimaanisha kuvuka vituo kadhaa vya ukaguzi kila siku.
Mnamo Machi 30, niliendesha baiskeli tena hadi kwenye kanisa la Baba Serhiy. Lakini, nilipofika, niligundua kwamba alikuwa amekamatwa pia na mamlaka ya Urusi.
Nilizifuta haraka jumbe zote alizokuwa amenitumia na nikiwa na jazba nikisubiri iwapo chocote kinaweza kutokea.
Usiku huo, alichapisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba alikuwa ameachiliwa bila kujeruhiwa, lakini katika ziara zangu zilizofuata katika kanisa lake niliona mtu aliyebadilika - alionekana amechoka na kukengeushwa.
Kadiri wiki zilivyopita, alizidi kuwa mbali nami na wengine waliomtembelea.
Hakwenda hata kanisanitena. Nilipompigia simu aliniambia kuwa kila kitu kiko sawa.
Lakini karibu mwisho wa Aprili, alianza kuchapisha kwenye mitandao ya kijamii tena.
Alifichua kwamba hakuweza tu kutoroka kutoka mjini Kherson, lakini pia alikuwa amedanganya katika ujumbe wa awali kutoka kwake.
Alisema Warusi wasiojulikana walimlazimisha kupiga magoti, kuweka kichwa chake kati ya magoti yao na kutishia kumbaka. Kwa madai kwamba alikubali kuwa msaliti.

"Kusema kweli, naona aibu," aliandika katika ujumbe wake. Tulianza kuhisi kwamaba tunafuatiliwa zaidi kutoka kila mahali.
Kwa kitendo cha uasi, mimi na Lidia tulisherehekea ukumbusho wetu kwa kuvunja hoteli iliyoachwa, ambako tulipiga picha na kula sahani za Kigeorgia tulizoleta.
Tunapanda paa na kuangalia mandhari ya kuvutia. Tuliona jiji letu katika mwanga mpya wa ajabu. Hata maelezo yasiyo na hatia yalionekana kuwa mabaya.
Vikosi vya Urusi viliharakisha kampeni yao ya kuondoa utambulisho wa Kherson nchini Ukraine.
Bendera na alama za Ukraine ziliondolewa, makaburi ya mashujaa wetu yaliharibiwa.
Mnamo Mei 6, mwanasiasa mkuu wa Kirusi, Andrey Turchak, alitembelea jiji hilo na akatangaza: "Urusi iko hapa milele. Naomba kusiwe na shaka juu ya hilo. Hakuna kurudi nyuma sasa." Yote hayo yalikuwa sehemu ya maandalizi ya sherehe za ushindi wa Jeshi Nyekundu dhidi ya Ujerumani ya Nazi mnamo Mei 9.
Niliwarekodi wakazi wa kawaida wa Kherson wakionyesha uungaji mkono wao kwa Warusi kwa kuvaa riboni za Saint George - nembo ya ushindi wa kijeshi wa Urusi.

Katika nyanja ya familia, shinikizo pia liliongezeka.
Shemeji yangu Vitaly alikuwa ametembelewa na Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB).
Aliniambia kuwa mmoja wa watu hao alimpa bomu, akavua pete ya usalama na kuondoka.
Aliporudi alimwambia kwamba ilikuwa "utani tu" huku akitabasamu.
Wakala mwingine wa FSB aliamuru Vitaly kuripoti na nyaraka zake ili yeye na Maryna waweze kuhamishwa hadi Crimea.
Bila shaka, hawakutaka kuhamishiwa Crimea mikononi mwa Warusi.
Tukio hilo lilituonyesha wazi jinsi hali ilivyokuwa tete kwetu.
Maryna na Vitaly walipakia vitu vyao na kujiandaa kuondoka siku iliyofuata, na tukatambua kwamba ilikuwa ni jambo la busara kwetu kwenda nao.
Tulifunganya virago vyetu kwa haraka. Tuliandika maelezo kumhusu Ksusha kwenye karatasi, ikiwa ni pamoja na ni nani anapaswa kumtunza ikiwa hatukunusurika, na tukaficha kijikaratasi hichoo kwenye kishikilia kadi ambacho tulimvisha shingoni.
Tulitoka kwa kasi katika msafara tukiwa na dada yangu, tukipita kwa woga kila kituo cha ukaguzi - kwa wasiwasi karibu na eneo la vita.
Familia hiyo hatimaye ilifika eneo salama.
Miezi mitano baadaye, familia hiyo sasa inaishi Kyiv.













