Shughuli za kilimo zinavyohatarisha ikolojia ya Ziwa Victoria

Maelezo ya video, Shughuli za kilimo zinavyohatarisha ikolojia ya Ziwa Victoria

Uchafuzi wa Ziwa Victoria: Wataalamu wa mazingira wanaonya kuwa shughuli za binadamu ikiwemo kilimo zinaendelea kuhatarisha mfumo wa ikolojia ndani na karibu na Ziwa Victoria nchini Tanzania.

Hii ni kutokana na kuongezeka kwa kemikali zinazotumika katika shughuli za kilimo kando ya mwambao wa ziwa. Mwandishi wetu Alfred Lasteck ametuandalia taarifa ifuatayo.