Mfereji wa Malacca: Njia ya bahari ambayo inaweza kusababisha usumbufu mkubwa duniani

Chanzo cha picha, Alamy
Iko maili mia chache, lakini kama patatokea janga la asili katika eneo hili la bahari, matokeo yake yatakuwa makubwa na kugusa dunia, anaandika Tom Ough.
Kila mwaka, takriban meli 90,000 hupitia katika njia hii nyembamba ya bahari ya Malacca Strait, inayounganisha Bahari ya Hindi na Pasifiki.
Mizigo yao - nafaka, mafuta ghafi, na kila bidhaa nyingine chini ya Jua - inajumuisha wastani wa 40% ya biashara ya kimataifa. Kuhusu meli hizi ni mojawapo ya njia za anga zenye shughuli nyingi zaidi duniani, lakini chini ya bahari, kuna safu nene za nyaya za mtandao wa internent ambazo uunganisha ulimwengu kimtanda.
Kwa pamoja, mambo haya hufanya Mlango-Bahari wa Malacca kuwa mojawapo ya sehemu muhimu zaidi ya uchumi wa dunia. Imeainishwa katika ripoti za Shirika la Biashara Duniani, Taarifa za Nishati za Marekani na Chatham House, taasisi ya masuala ya nje yenye makao yake makuu mjini London kama sehemu nyeti zaidi.
Yote ni kusema: Ni mkondo mzuri. Lakini wasiwasi ikiwa kitu kitatokea. Watafiti wanaonya kwamba ni suala la muda tu kabla ya maafa ya asili kama tetemeko la ardhi au volcano kupiga eneo hilo - na likitokea, tunaweza kutarajia athari kubwa na mabaya ulimwenguni.

Chanzo cha picha, Alamy
Usumbufu wa njia kuu za biashara ni tatizo linalofahamika vyema, kutokana na uhalifu au makosa ya kibinadamu.
Uharamia umekuwa ukiharibu eneo hilo kwa muda mrefu, lakini eneo la bahari linalosimamiwa kwa ushirikiano na Indonesia, Malaysia, Singapore, na Thailand, kwa ujumla limedhibitiwa.
Bado, sio kawaida kwa meli kugongana hapa. Lakini kwa umbali wa maili 1.7 (km 2.7) wenye wembamba zaidi, mkondo wake sio mwembamba kiasi cha meli ya kontena kushindwa kupita.
Hatari kubwa zaidi kwa Mlango-Bahari wa Malacca, ambao hutenganisha Rasi ya Malay na kisiwa cha Indonesia cha Sumatra, ni kwamba uko katika ulimwengu wa asili.
Kati ya masuala mengi yanayotuvia katika eneo hilo zaidi ni ile inayokusanya volkano hai duniani na matetemeko ya ardhi ya hivi majuzi.

Chanzo cha picha, Alamy
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Hatari kubwa zaidi kwa Mlango-Bahari wa Malacca, ambao hutenganisha Rasi ya Malay na kisiwa cha Indonesia cha Sumatra, ziko katika eneo la asili la ulimwengu.
Ni eneo lenye kuvutia kwa majanga ya asili. Kando ya pwani ya Sumatra na sehemu ya kusini zaidi ya Java na Sunda, ni eneo lenye kuvutia matetemeko ya ardhi, na volkano kadhaa.
Kwenye maeneo hayo kumelipuka volkano mbili hivi karibuni. Katika Mlango-Bahari wa Sunda, unaotenganisha Java na Sumatra, ni Krakatoa, na magharibi zaidi ni ule wa Tambora, ambao mlipuko wake wa mwaka wa 1815 ulisababisha kudumaa kwa mazao katika maeneo mpaka ya mbali kama Ulaya na Marekani mashariki.
Iwapo moja kati ya maeneo haya ya volkano ikalipuka kama kwa mfano Java, Indonesia – huenda ikasababisha madhara makubwa zaidi ulimwenguni.
Tetemeko kubwa la ardhi karibu na eneo hilo linaweza kuwa tishio kwa kiwango sawa. Inaweza kusababisha tsunami kupiga mkondo huo, kama Tsunami iliyotokea mwaka 2004, Disemba 26.
"Mlipuko wa Tonga" - mnamo Januari 2022 - "ilikuja na mikondo ya tope iliyokata nyaya, na kusababisha kukatika kwa mtandao wa kikanda. Mikondo ya uchafu pia huziba nyaya hizo, na kufanya urejeshaji wao kuwa mgumu zaidi, anasema Lara Mani, mtaalam wa volkano kutoka Chuo Kikuu cha utafiti cha Cambridge.
Mani anaangazia kukatika kwa nyaya kadhaa za mtandao chini ya bahari kutokana na tetemeko la ardhi la Taiwan mwaka wa 2006, na kuacha waya moja tu inayofanya kazi ikiunganisha Hong Kong na dunia nzima.
"Ilichukua siku 45 kukarabati nyaya zingine, na ilikuwa bahati sana kwamba waya mmoja ulikuw aunafanya kazi. Hebu fikiria siku 45 bila mawasiliano kati ya Hong Kong na maeneo mengine duniani, ingekuwa janga." Anaendelea, akiongeza sio tu kwa Hong Kong lakini kwa ulimwengu wote.
Hong Kong, kama Singapore, ni kitovu cha kifedha ambacho kutoweka kwake kunaweza kusababisha uchumi kuyumba duniani kote.

Chanzo cha picha, Alamy
Kwa hivyo nini cha kufanywa kukwepa hatari yoyote katika eneo hili? Hakuna tunachoweza kufanya ili kudhibiti matetemeko ya ardhi. Mamlaka za bahari na UNESCO wameweka mifumo ya kutoa tahadhari ya mapema kwa matukio kama vile tsunami, na kuna huduma ya kuonya usafirishaji baharini kutokana na majanga ya hali ya hewa au kijiolojia.
Japani ndiye mratibu mteule wa eneo hilo linalojumuisha Mlango-Bahari wa Malacca. Kuhusu volkano, siku moja inaweza kuepusha milipuko kwa kudhibiti 'magma' iliyo chini yake.
Kwa sasa, ni lazima tuwe bora sio tu kwa ufuatiliaji wa volkano - hata utoaji wa taarifa mapema kabla ya mlipuko huleta tofauti kubwa. Kama Mani anavyoonya, Indonesia ina "volkano nyingi kuliko hata namna unavyoweza kutikisa fimbo yako, na nyingi kati hizo volkano sisi kama wataalamu wa volkano duniani - "hatujazipa nguvu ya kuzizingatia ipasavyo."












