'Nilichimba madini kwa miaka sita wakijua mimi ni mwanaume'

'Nilichimba madini kwa miaka sita wakijua mimi ni mwanaume'

Pili Hussein mwanamke kutoka Tanzania alitamani kujiimarisha kimaisha na kupata utajiri kupitia madini, lakini kwa kuwa wanawake hawakuwa wanaruhusiwa kwenye migodi hiyo alivalia mavazi kama mwanamume na kuwadanganya wafanyakazi wenzake kwa miaka kadhaa kama yeye ni mwanaume.

Wakati wote wa kazi hiyo alikua akijulikana kama 'Mjomba Hussein'.

Lakini je, aligundulika vipi kama yeye ni mwanamke?

Mwandishi wa BBC Munira Hussein alimtembelea nyumbani kwake Mererani Arusha na kuandaa taarifa ifuatayo.