‘Napenda kufanya mazingaombwe kuliko kazi ya ukufunzi’

Pastory Pascal maarufu kamą @boomtz_ ni msanii wa sanaa ya mazingaombwe ambaye amekuwa akipata wafuasi kila uchwao kutokana na aina ya mazingaombwe yake kuwa ni yale yaliyochangana na vichekesho.

Licha ya kuwa ni mwanamazingaombwe lakini kijana huyu pia ni mkufunzi wa chuo akiwafundisha waalimu somo la sayansi.

Je unadhani kati ya Sanaa ya mazingaombwe na ufundishaji anapendelea nini zaidi.

Mwandishi wa BBC @frankmavura amekutana naye jijini Dar es Salaam na kutuandalia taarifa hii.