Kwa nini majina ya watoto yasiyo ya kawaida yanaongezeka?
Chanzo cha picha, Getty Images
Chanzo cha picha, Getty Images
Majina yasiyo ya kawaida ya watoto yanaongezeka kote ulimwenguni, hata katika jamii nyingi za kitamaduni.
Kwa nini wazazi wanazidi kudhamiria kutaja Watoto wao majina ya kipekee.
Ziara yangu ya kwanza nchini Pakistani iliondoa mawazo yoyote ya thamani niliyokuwa nayo kuhusu upekee wa jina langu.
`Wakati kuna kuwa na hamu kubwa ya kuhakikisha upekee huo huko California, hapa, ilionekana nikukutana na Aysha, Aisha au Aisha kila kona.
Ni kama mulikuwa mumefungua kitabu cha majina ya watoto na hata humukutazama zaidi ya 'A',". ningewaambia wazazi wangu, na kuapa kwamba nitakapokuwa na watoto, ningechagua jina la kipekee.
Na hivyo ndivyo nilivyofanya, nikamtaja binti yangu Sidrat-ul-Muntaha, kutokana na mti wa ajabu unaoaminika kuashiria mpaka wa mwisho kabisa katika mbingu ya saba - kihalisia ni eneo la mwisho na hakuna mtu anayeweza kupita hapo.
Kumpa mtoto jina ni mchakato unaosababishwa na hisia.
Wazazi wana wasiwasi kuhusu athari ya muda mrefu ya jina la mtoto, na wanahisi wanahitaji kufanya kazi bora zaidi katika kumpa mtoto jina kwa ajili ya mafanikio.
Hiyo ni kwa sababu tunajua majina ni muhimu.
jina letu ndio utambulisho wetu, huathiri dhana potofu za majina, huenda kukaamuru aina za kazi tunazofuatilia na hata kutabiri mafanikio ya kitaaluma.
Mitindo inayohusu jinsi wazazi wanavyochagua majina kwa watoto wao ni zao la tamaduni zetu zilizokuwepo na zinazoendelea.
Hubadilika kama matarajio ya watoto yanavyobadilika.
Utafiti unaonyesha kuongezeka kwa umaarufu wa majina ya kipekee ya watoto unaonyesha kuhama kutoka kwa umoja hadi jamii za watu binafsi, na hutoa vidokezo muhimu vya muktadha kuhusu wazazi, wanataka watoto wao wawe nani.
Duniani, inaonekana, wazazi wanazidi kuthamini majina ya kipekee ili kuwasaidia watoto waonekane tofauti, badala ya kuwapaa tu majina ili awe ni somo yake fulani.
Kutoka kwa mila hadi kujieleza
Katika karne zilizopita, upatanifu wa majina unaotokana na utamaduni ndio ulikuwa msukumo mkuu, anaeleza Laura Wattenberg, mwanzilishi wa namerology.com na mwandishi wa The Baby Name Wizard.
"Wazazi walifanya tu kile ambacho kilikuwa kimefanywa siku zote, asema, akionyesha kwamba huko Uingereza, John na William, kwa mfano, walikuwa majina ya wavulana yaliopendwa zaidi kutoka miaka ya 1200 hadi 1930.
"Kulingana na [takwimu] zilizokusanywa na mwanauchumi Douglas Galbi, katika miaka ya 1600, majina matatu ya kwanza ya wavulana na wasichana yaliyopendwa zaidi yalichukua nusu ya idadi ya watu [wa Uingereza]," aeleza.
Hii ni kwa sababu mikataba ya majina ilianzishwa katika mahusiano ya kidini na mababu.
Kwa mfano, majina ya kimaandiko yalikuwa maarufu, na Wapuriti wa Kiingereza ambao pia walikuwa Wanamapinduzi wa kidini wakati fulani waliwaita watoto wao kutokana na sifa za maadili, kama vile Imani au Rehema.
Chanzo cha picha, Getty Images
Vile vile, Waislamu katika nchi za Kiarabu na Kusini mwa Asia walisifu udini.
Majina ya jadi ya Kiislamu yanajumuisha watu mashuhuri wa kihistoria katika Uislamu (kama vile Muhammad, baada ya Mtume SAW, watu wa zama zake, Umm-ul-Momineen au wake zake - akiwemo Hazrat Aisha RA - na makhalifa wa dola za Kiislamu).
Mara nyingi, majina yalisisitiza kujitolea kidini, kama vile mojawapo ya majina 99 ya Mwenyezi Mungu yenye neno lililotangulia Abdul, likimaanisha mtumishi wa.
Utamaduni wa kutaja majina ya Waarabu pia ulikuwa na nasaba iliyokita mizizi, na majina yakitanguliwa mara kwa mara na maneno kama vile Bint-e- (binti ya), Umm-e- (mama yake), Abu (baba yake) au Ibn (Mwana wa).
Kulingana na kasi ambayo mikoa tofauti ilikua, sio mila hizi zote zilidumu.
Kudhoofisha uhusiano wa kitamaduni na idadi kubwa ya watu karibu na Mapinduzi ya Viwandani kulifanya chaguo za wazazi vijana kutoamriwa na mila na desturi za kifamilia katika ulimwengu wa Magharibi, anaelezea Wattenberg.
"Majina yalizidi kuwa njia ya kujieleza ... utamaduni wote ulihamia kwenye sherehe kubwa ya uhuru wa kibinafsi na ubinafsi."
Utafiti wa hapo awali umegundua kupungua kwa kasi kwa majina ya kawaida nchini Marekani kutoka miaka ya 1950, haswa kutoka 1983, na uchunguzi wa hivi karibuni wa kiwango cha juu uliochambua majina ya watoto milioni 348 wa Marekani katika miaka 137 (1880 hadi 2017) ulionyesha kuwa waliozaliwa kati ya mwaka 1946 na 1964, waliongeza idadi ya majina mapya kwa watu elfu mara nne kwa wavulana na mara 2.75 kwa wasichana.
"Waliozaliwa kati ya mwaka 1946 na 1964, walikuwa wazazi wa kwanza ambao walitaka kuwa watu wazuri, na ambao walitaka watoto wao wawe wazuri pia," anasema Pamela Redmond, ambaye kitabu chake cha mwaka 1988 Beyond Jennifer & Jason alichunguza kikundi hicho kama kizazi cha kwanza kukataa kutaja majina ya watoto wao kwa kuzingatia makabila na dini kama ilivyokuwa zamani.
Na kwa shauku iliyoimarishwa hasa baada ya kuingia kwa intaneti katika miaka ya 1990, waliozaliwa kati ya miaka ya 1980 na 1990 walipiga hatua zaidi.
"[Wazazi hawa] walizoea mfano wa jina la mtumiaji - kitambulisho chako cha kipekee katika mfumo wa kijamii," anasema Wattenberg.
"Wazazi wangeandika jina kamili walilokuwa wakizingatia kwenye mitandao na kuwa na wasiwasi kwa sababu 'lilishachukuliwa'.
Miaka ya 1990 pia ilileta mtindo mpya: takwimu za majina ya watoto … Uorodheshaji wa kila mwaka wa majina maarufu ulifanya watu kuhisi ushindani.
Leo hii, wazazi huonyesha mtindo na maadili yao kwa majina, anaeleza Redmond, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Nameberry, mshauri wa majina ambayo huwapa wazazi mwongozo wa jinsi ya kuchagua jina jipya.
"Tunasikia wazazi wengi wakisema wanataka kuwapa wana wao majina yasiyo ya kijinsia ili kuashiria maadili ya wanawake, au kuheshimu familia kwa njia inayoendana na mitindo ya."
Hata Japani, ambayo imekuwa na utamaduni wa kijami kwa karne nyingi, inaonyesha kuhama kutoka kwa mila za kutaja majina.
Kulingana na utafiti wa mwaka 2021 uliochanganua majina 8,000 ya watoto kati ya mwaka 2004 na 2018, kiwango cha majina ya kipekee kinaongezeka nchini Japani - na ni kiashirio cha kuongezeka kwa ubinafsi.
Kwa ujumla, wazazi wamekuwa na mtindo wa kubadilisha matamshi, maadhishi na kadhalika ili kutafuta upekee katika majina.
Nchini Pakistani, kwa mfano, wakati udini bado unatawala, vitendo vingi zaidi vya ibada vinasimama kama majina, kama vile Azaan (wito wa sala) au Ayat (aya ya Kurani), badala ya majina muhimu ya kihistoria ya Mitume, ikipendekeza kwamba wazazi kufikiri zaidi kutafuta majina ambayo bado ni ya kidini, lakini si ya kawaida.
Chanzo cha picha, Thinkstock
Tafiti kutoka China pia zinaonyesha majina ya kipekee ya watoto ni mojawapo ya njia nyingi za kutimiza upekee kunakoongezeka, kulikotokana na uhuru, ikiunganishwa na kupungua kwa umuhimu wa mila na desturi za kitamaduni za Kichina.
Mitindo hii inapojitokeza, je, tunapaswa kutarajia kuongezeka kwa majina mengi ya asili na yasiyo ya kawaida?
Hata hivyo kuna wake wanaodhani kwamba mwelekeo kuelekea majina yasiyo ya kawaida hatimaye utafikia mwisho.
Na kutafuta majina ya kipekee kunaweza kusiwe jibu au tikiti ya mafanikio ambayo wazazi wanataka iwe hivyo.
"Wazazi wanahisi kwamba kuchagua jina la pekee kutampa mtoto wao faida maishani. Ni msukumo wa upendo, lakini kiutendaji haiko wazi kuwa inafanya kazi kwa njia hiyo,"anasema Wattenberg, kwa sababu baada ya yote, "Maarufu inamaanisha kupendwa - na majina tofauti sana yanaweza kuwa ya mgawanyiko.
Watu wanaweza kuelekeza watu mashuhuri waliofanikiwa wenye majina ya kipekee, lakini kwa kila Madonna na Beyoncé kuna Michael Jackson, Emma Thompson, Sam Smith na Elizabeth Taylor," anamalizia Wattenberg.
Hatimaye, kwa wazazi, kumpa mtoto jina ni tendo la upendo, linaloathiriwa na ndoto za kibinafsi na kutaka kuendeleza utamaduni wa maadili.
"Wazazi hutujia ili kupata usaidizi wa kupata jina linalofaa kwao, zaidi ya lile ambalo ni tofauti na mtu mwingine yeyote ,"asema Redmond.
Habari kuu
Gumzo mitandaoni
Zinazovuma zaidi
Haipatikani tena