Muigizaji nguli Marekani Cicely Tyson afariki dunia

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Mwaka 2018, Cicely Tyson alikuwa mwanamke mweusi wa kwanza Mmarekani kupokea tuzo ya heshima ya Oscar
Muda wa kusoma: Dakika 2

Muigizaji nguli wa Marekani Cicely Tyson - ambaye alifahamika zaidi kwa jinsi alivyomwakilisha Mmarekani mweusi ambaye ni jasiri, amefariki akiwa na umri wa miaka 96, meneja wake ameeleza.

Sababu ya kifo chake hakijaelezwa mpaka sasa.

Mbunifu huyo wa zamani wa mitindo ambaye aliigiza kwa kipindi cha miongo saba.

Nguli huyo wa filamu alishinda tuzo mbili za Emmys , kutokana na filamu yake ya haki za raia ya mwaka 1974 ambayo iligusia historia ya wasifu wa Bi. Jane Pittman.

Alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kufanya jukumu la kuwa muigizaji nyota wa maigizo ya Luninga mnamo miaka ya 1960.

Tyson alipewa medali ya Uhuru kutoka kwa rais mwaka 2016, Rais Barack Obama alisema licha ya mafanikio yake kama muigizaji ,lakini alifanya jukumu kubwa katika historia.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Tyson alibadilisha mtazamo hasi kuhusu mwanamke mweusi , kwa kuwa anacheza nafasi ya ujasiri na chanya .

"Nilifanikiwa kumuongoza Bi. Tyson kwa zaidi ya miaka 40, na ilikuwa ni heshima kubwa kwake pamoja na baraka," meneja wake Larry Thompson alisema Alhamisi wakati akitangaza kifo cha bi. Tyson.

"Namkumbuka Cicely kama mapambo ya krismasi kupitia tasnia yake na maisha yake binafsi.

Leo tunamvisha taji nyota, juu ya mti," meneja aliongeza kusema kuwa bi. Tyason alikufa kwa amani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lupita Nyong'o akiwa na Tyson

Aliandika : "'Tafadhali ,'nilisema usicheke, jihisi kuwa na uhakika kulikuwa na mtu ambaye anaongea mambo yasiyoeleweka.

Ulipataje hii namba kwanza? Alijaribu kunishawishi kuwa suala alilolitaka lilikuwa la kweli lakini sikusikia'."

Alieleza jinsi alivyokutana na mume wake , Miles Davies, miaka ya 60 baada ya mwanaume huyo kubisha hodi katika nyumba ya jirani yake Diahann Carroll', ambako Tyler alikuwa mgeni.

Alionekana akiwa anataka kusaidiwa sukari.

Alioana na mume wake kuanzia mwaka 1981 mpaka 1988.

Chanzo cha picha, Getty Images

Alizaliwa New York mjini Harlem, alikuwa na wazazi ambao walikuwa wakristo katika kisiwa cha Nevis.