DJ Dolla: 'Kwa nini niliamua kuwa DJ'

Maelezo ya video, DJ Dolla: 'Kwa nini niliamua kujitosa kwenye burudani'

Lightness Lucus almaarufu DJ Dolla mwenye miaka 28 mkazi wa jijini Arusha alichana na uanamitindo na kujitupa kwenye uburudishaji kama DJ kazi ambayo anasema inapewa sifa mbaya na jamii kwani wafanyao wanaonekana kama hawana maadili.

Kwa kipindi cha miaka sita ambacho amekua DJ toka alipohitimu mafunzo ya miezi mitatu Dj dolla hufurahia zaidi kupiga nyimbo za zamani na afro pop.

Akiwa jijini Arusha Eagan Salla alizungumza naye na hii hapa ni simulizi yake.

Video: Eagan Salla