Mwili wa Hayati John Pombe Magufuli waagwa Zanzibar

Mwili wa Hayati John Pombe Magufuli umeagwa leo kisiwani Zanzibar na kesho unatarajiwa kuagwa mkoani Mwanza.

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu and Lizzy Masinga

  1. Mpaka hapa tumefikia mwisho wa matangazo ya moja kwa moja ya kurasa ya BBC Swahili, Asante na tukutane kesho.

  2. Simulizi ya koti aliloachiwa mama,

    NASRA NASSOR

    Chanzo cha picha, NASRA NASSOR

    Taswira ya picha hii ambayo imepata umaarufu mkubwa nchini Tanzania, imebuniwa na kupigwa picha Bernad Atilio na imechorwa na mchoraji kupitia sanaa ya urembo Nasra Nassoro.

    Bwana Bernad anafafanua kuwa picha hii inayomwakilisha Rais wa Tanzania, mama Samia Suluhu Hassan atakavyoweza kuvaa viatu pamoja na koti la majukumu ya Urais aliyoachiwa na Rais Magufuli.

    Kwa mujibu wa mchoraji Nasra, anasema katika picha hii kuna koti na viatu ambavyo vinawakilisha baba aliyeondoka na kumuachia mama majukumu yake yote ambayo alikuwa akiyafanya.

    Pembeni kuna mtoto anamtazama mama, Hii ikiwa inawakilisha wananchi wote wa Tanzania.

    Na wakati huo huo mtoto akiwa ameshika jembe linalowakilisha utendaji kazi na macho yote yakimwangalia mama kujua nini ategemee.

    Lakini picha hii inaonesha kiza kinene na mwanga ukimmulika mama kwa mbali.

    Hii ikiwa ishara ya matumaini kwa watanzania yakiwa kwa mama kujua namna watakavyoishi.

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

    Wachoraji wa picha hii wanasema wanajivunia sana kazi hii waliyoifanya kwa kupeleka ujumbe ambao ndio hiki kinachoendelea Tanzania kwa sasa na mama amevaa koti na viatu vya baba.

    Na mama mwenyewe ametuhakikishia kwa kusema 'Yeye ndiye Rais.'

  3. 'China imempoteza rafiki' asema Rais Xi Jinping

    China

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Jamhuri ya watu wa China Xi Jinping amemtumia barua Rais wa Tanzania ya salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli na pia kumpongeza Rais Samia kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Katika barua hiyo ,Rais Xi Jinping amesema amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha Rais Magufuli.

    Amesema kwa niaba ya watu wa China anatoa salamu za rambirambi kwa familia na Watanzania kwa ujumla kufuatia msiba huu.

    Ameongeza kusema kuwa Rais Magufuli alikuwa kiongozi wa Afrika na Tanzania aliyelinda maslahi ya nchi yake dhidi ya mataifa ya kigeni na kuendeleza taifa lake katika uhalisia.

    "Kifo cha Hayati Magufuli ni pigo kwa watanzania na pia China imempoteza rafiki wa kweli", amesema Xi Jinping.

    Rais Xi Jinping amesema China inajivunia urafiki wake na Tanzania na imehaidi kuendelea kushirikiana na Tanzania kwa maslahi ya pande zote.

  4. Mwanachama wa Chadema alipa faini kwa uchochezi mtandaoni

    Mwanachama mmoja wa chama cha upinzani nchini Tanzania, Yericko Nyerere amelipa faini ya shilingi milioni tano badala ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la kuandika ujumbe wa uchochezi mtandaoni, gazeti la Mwananchi limeandika.

    Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimhukumu mwanachama huyo wa chama cha upinzani kwa kosa la kuchapisha maneno ya uchochezi katika mtandao wa kijamii wa Facebook yanayotishia kuvunja amani ya taifa hilo.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Nyerere anakabiliwa na shitaka moja la kusambaza taarifa zinazodaiwa kuleta taharuki kwa watu kupitia akaunti yake ya kijamii ya Facebook, kitendo anachodaiwa kukifanya Mei 28, 2017 mkoani Dar es Salaam.

    Faini hiyo imelipwa leo baada ya kuhukumiwa na mahakama hiyo.

  5. Hakuna vitanda vya ICU -Muungano wa madaktari Kenya wasema

    kenya

    Chanzo cha picha, Reuters

    Muungano wa madaktari nchini Kenya (KMPDU) umeonya kuwa hakuna nafasi katika vyumba vya wagonjwa walio katika hali ya mahututi yaani ICU katika maeneo yote nchini humo.

    ‘Idadi ya maambukizi inaongezeka na wahudumu wa afya hawajaachwa na janga hilo. Madaktari 10 hadi sasa wamelazwa," Katibu mkuu wa muungano huo Chibanzi Mwachonda amesema siku ya Jumanne.

    Mwachonda amesema Kenya sasa inahitaji wahudumu zaidi wa afya kwa sababu madaktari wengi wamelazwa baada ya kuambukizwa virusi vya Corona .

    " Uhaba huu wa madaktari ni hatari sana kwa sekta ya afya .Tunahimiza wizara ya Afya na Hazina ya kitaifa kuharakisha utoaji wa mikataba kwa waudumu 156 waliopewa kazi katika vituo vya kuwatenga wagonjwa nchini kote’ ameongeza kusema katibu huyo.

    Amewapa himizo wananchi na viongozi wa kisiasa kuzingatia kanuni za kukabiliana na Covid-19 ili kuokoa maisha ya wahudumu wa afya.

    Kuhusu chanjo, Mwachonda amesema wafanyakazi wa afya wameogopa kuchukua chanjo hiyo kwa sababu ya ukosefu wa uhamasishaji. Serikali ilipokea dozi milioni 1.02 za chanjo ya AstraZeneca mnamo Machi 3 kupitia Covax na dozi 100,000 zaidi kutoka kwa Serikali ya India. Kufikia Jumatatu, zaidi ya Wakenya 40,000 walikuwa wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo hiyo huku dozi ya pili iikitarajiwa kutolewa baada ya wiki nane

  6. Shirika la ndege la Kenya lapata hasara ya Dola milioni 332

    Airteamimages

    Chanzo cha picha, Airteamimages

    Kenya Airways imepata hasara ya dola milioni 332 mwaka wa 2020, ikilinganishwa na hasara ya Dola milioni $ 118 mwaka uliotangulia. Ongezeko la hasara hiyo kwa asilimia 179 lilitokana na kuvurugika kabisa kwa safari za anga za kimataifa kwa sababu ya athari mbaya za janga la COVID-19.

    Shirika hilo limeripoti kuwa idadi ya abiria ilipungua kwa asilimia 65.7 hadi milioni 1.8 kwa mwaka, na kusababisha hasara ya mapato ya dola milioni 473.

    Mwenyekiti wa Kenya Airways Michael Joseph amesema, "Mlipuko wa COVID-19 mnamo 2020 ulikuwa zaidi ya utabiri wa mtu yeyote na athari zake kwa sekta ya usafiri wa angani zinatarajiwa kuendelea kwa miaka miwili hadi mitatu ijayo."

    Mwaka jana , Kenya Airways iliwaachisha kazi wafanyakazi 650 na kupunguza mishahara ya wafanyakazi waliobakia na kuzibadilisha ndege kadhaa za abiria kuwa za kubeba mizigo.

    Shirikisho la Kimataifa la Usafiri wa Anga, IATA, linatabiri kuwa mashirika ya ndege ya Afrika yanaweza kupoteza hadi $ 6 bilioni katika mapato, na kuathiri kazi za sekta ya usafiri wa anani zipatazo 172,000.

  7. Kifo cha Magufuli: Mwanza yawataka wazee, watoto wafuatilie kwa njia ya televisheni na redio

    Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela

    Chanzo cha picha, John Mongela/Twitter

    Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amewaomba wazee kufuatilia shughuli ya kumuaga Hayati Magufuli kwa njia ya kufuatilia vyombo habari badala ya kwenda uwanjani.

    Amewataka pia wazazi jijini humo kutowaruhusu watoto, badala yake wasaidiwe kufuatilia kupitia kwenye runinga.

    Maandalizi ya kuupokea mwili wa hayati Magufuli yanaendelea kwenye uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majukwaa, mahema ya nguvu kazi pamoja na kamati mbalimbali.

    Maandalizi ya kumpokea Hayati John Magufuli

    Bw.Mongela amesema kesho milango itafunguliwa saa kumi alfajiri ili kuwapatia watu muda wa kutosha kuingia uwanjani bila kusukumana .

    Maandalizi ya kumpokea Hayati John Magufuli

    Mwili wa hayati Magufuli utawasili uwanja wa ndege wa Mwanza ukitokea Zanzibar kesho saa moja asubuhi na unatarajiwa kupokelewa na maelfu ya Watanzania na kisha kupelekwa uwanja wa CCM Kirumba kwa heshima za mwisho.

    Mwili wa Hayati Magufuli utazungushwa maeneo mbali mbali jijini Mwanza kuwapa nafasi wakazi kutoa heshima za mwisho.

  8. Uchunguzi kuhusu kifo cha mpinzani wa Denis Sassou Nguesso kuanza

    Ofisi ya mwendesha mashtaka ya Bobigny nchini Ufaransa imetangaza kuanza uchunguzi kuhusu chanzo cha kifo cha mpinzani wa Congo,Guy Brice Parfait Kolelas.

    Kwa mujibu wa mamlaka za Congo alikutwa na maambukizi ya Covid 19 siku ya Ijumaa,juma lililopita.

    Guy Brice Parfait Kolelas alikuwa mgombea wa nafasi ya urais siku ya Jumapili, Machi 21.

    Guy Brice Parfait Kolelas, 61, alipoteza maisha siku ya Jumapili kwenye ndege ya matibabu iliyompeleka jijini Paris, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kampeni Christian Cyr Rodrigue Mayanda .

    Kwa mujibu wa taarifa ya kwanza iliyotolewa na mamlaka za Congo, Guy Brice Parfait Kolélas, alikutwa na maambukizi ya virusi vya corona, alipokuwa akilalamika kuugua malaria.

    Alilazwa hospitalini Brazzaville, hali yake ikielezwa kuwa mbaya sana Jumamosi, alichapisha video akiwa kwenye kitanda akisema kwamba alikuwa akipambana na kifo.

    Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Bobigny huko Ufaransa ilitangaza kuanza uchunguzi wa jinai juu ya sababu za kifo cha mpinzani ambaye mwili wake bado haujarejeshwa.

    Guy Brice Parfait Kolelas ndiye aliyekuwa mpinzani mkubwa wa Denis Sassou Nguesso wakati wa uchaguzi wa urais wa Machi 21.

  9. Mwili wa Hayati Magufuli wawasili uwanjani

    Mwili ukiingia uwanja wa Amani

    Mwili wa Hayati John Magufuli umewasili katika uwanja wa Amani tayari kwa kuagwa na Wazanzibari.

    Shughuli ya kuaga mwili itaongozwa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi.

    Mwili wa Hayati Magufuli uwanjani
    Mwili wa Hayati Magufuli uwanjani
  10. Idadi ya watu waliokufa katika shambulio la kijiji Niger yafikia 137

    Niger ni sehemu iliyo chini ya muungano wa nchi zinazoiunga mkono Ufaransa katika ukanda wa Sahel

    Chanzo cha picha, AFP

    Serikali nchini Niger inasema kuwa idai ya watu waliotambuliwa kuuawa katika shambulio la Jumapili linaloshukiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Islamic State ni 137.

    Vijiji vitatu vililengwa katika shambulio hilo, karibu na mpaka na nchi jirani ya Mali.

    Niger inakabiliwa na misururu ya mashambulio ya kushtukiza yanayofanywa na wanamgambo wa Kiislamu ambao hufanya uvamizi wa kushambulia na kutoweka dhidi ya vijiji vilivyo mbali kwa kutumia pikipiki na magari ain pick-up.

    Imebainika kuwa shambulio la Jumapili dhidi ya vijiji vilivyopo kwenye mpaka wa Nijer, Mali na Burkina Faso lilikuwa baya –ambapo raia zaidi ya 130 waliuawa.

    Ramani

    Kumekuwa na mashambulio ya aina hii katika eneo jingine la mapambano ambapo wanajeshi wa Mali waliuawa wiki moja kabla.

    Niger ni sehemu iliyo chini ya muungano wa nchi zinazoiunga mkono Ufaransa katika ukanda wa Sahel unaofahamika kama G5.

    Kikosi cha wanajeshi 1,200 kutoka jeshi la Chad, kinachotazamwa kama kikosi chenye nguvu zaidi, kimepelekwa kusaidia kukabiliana na tishio la mashambulizi hayo ya wanamgambo.

  11. Wazanzibari wajitokeza uwanja wa Amani kumuaga Hayati Magufuli

    Raia wa Zanzibar wajitokeza uwanja wa Amani

    Viongozi wa serikali na dini mbalimbali pamoja na wananchi tayari wamefika katika viwanja vya Amani Karume Kisiwani Unguja.

    Mwili utakapowasili shughuli hii ya kuaga mwili wa hayati Rais Magufuli itaanza rasmi ikiongozwa na Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi.

    Mwili wa Hayati Magufuli ukisubiriwa uwanja wa Amani
    Wanajeshi wakisubiri kuwasili kwa Hayati Magufuli uwanja wa Amani Zanzibar

    Mwili unapita kwenye maeneo mbalimbali ya mitaa wakati ukielekea uwanja wa Amani kwa ajili ya kuagwa.

  12. Viongozi wa dini wafanya maombi maalum mjini Chato,

    Viongozi wa dini wakisali

    Viongozi wa dini mbalimbali wafanya maombi maalumu mjini Chato kwa ajili ya kumuombea aliyekuwa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli.

    Maelezo ya video, Viongozi wa dini mbalimbali wafanya maombi Chato
    Raia wakisali mjini Chato

    Viongozi mbalimbali wa kidini wanamkumbuka rais Magufuli ambaye ni mzawa wa mjini Chato kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu na ukaribu aliokuwa nao na viongozi wa dini mbalimbali.

  13. Bendera ya Umoja wa Mataifa kupepea nusu mlingoti Machi 26

    Bendera ya Umoja wa Mataifa

    Chanzo cha picha, Umoja wa Mataifa

    Bendera ya Umoja wa Mataifa itapepea nusu mlingoti kwenye makao makuu yake Ijumaa Machi 26 kumuenzi aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli, kufuatia kifo chake Machi 17.

    Ofisi ya Itifaki imesema ofisi zote za Umoja wa Mataifa duniani zimehimizwa kufanya hivyo pia.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  14. Mwili wa Hayati Magufuli wawasili uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume

    Msafara uliobeba mwili wa Hayati Magufuli

    Chanzo cha picha, Habari Maelezo Tanzania

    Mwili wa Hayati Magufuli wawasili uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume.

    Raia visiwani Zanzibar wataungana na Watanzania wenzao kumuaga Hayati John Pombe Magufuli.

    Hayati Magufuli ataagwa katika uwanja wa Amani.

    Mwandishi wa BBC Halima Nyanza amesema mapema asubuhi watu walikuwa wakiingia kwa wingi katika uwanja huo, tayari kwa shughuli hiyo.

    Awali alipokuwa akizungumza na BBC, Mbunge wa Afrika Mashariki, Dkt Abdulah Makame alisema mwili utalakiwa na Rais wa Zanzibar, Dkt Hussein Ali Mwinyi katika uwanja vya ndege wa Abeid Aman Karume.

    Mwili utapita kwenye maeneo mbali mbaliya mitaa wakati ukielekea uwanja wa Amani.

  15. Msafara wa mwili wa hayati John Magufuli waelekea Zanzibar

    Msafara ukielekea Uwanja wa Ndege Dodoma kwa ajili ya safari ya Zanzibar

    Chanzo cha picha, habari maelezo

    Maelezo ya picha, Msafara ukielekea Uwanja wa Ndege Dodoma kwa ajili ya safari ya Zanzibar
    Msafara ukielekea Uwanja wa Ndege Dodoma kwa ajili ya safari ya Zanzibar

    Chanzo cha picha, Habari maelezo

    Maelezo ya picha, Msafara ukielekea Uwanja wa Ndege Dodoma kwa ajili ya safari ya Zanzibar
    Maelfu ya raia walisimama kando ya barabara kuuaga mwili wa John Pombe Magufuli

    Chanzo cha picha, habari maelezo

    Maelezo ya picha, Maelfu ya raia walisimama kando ya barabara kuuaga mwili wa John Pombe Magufuli
  16. Natumai hujambo . Ni siku nyengine ambapo tutaendelea kukupasha kuhusu kifo cha rais John Pombe Magufuli Moja kwa moja