Je ni lazima kwa tungo kuwa na aina fulani ya maneno ili kupendwa na mashabiki wa muziki?

Maelezo ya sauti, 'Tofauti ya mwanamuziki na mwandishi wa vitabu ni nini?'

Maelekezo mpya yaliyotolewa na Baraza la sanaa Tanzania (Basata) kuhusiana na upitishwaji wa nyimbo za wasanii yameibua gumzo katika mitandao na kila kona nchini Tanzania.

Baadhi ya wasanii wanasema hatua hiyo itawarudisha nyuma katika fani ya muziki wao huo wa Bongoflavor.

Je ni lazima kwa tungo kuwa na aina fulani ya maneno ili kupendwa na mashabiki wa muziki?

Mhariri mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania Oni Sigala anafafanua msingi wa kauli yake kwamba pana sintofahamu katika tungo za baadhi ya wasanii wa Tanzania.

Jitihada za kuwatafuta baraza la sanaa, hazikufanikiwa kupata ufafanuzi zaidi juu ya suala hili.

Mwandishi wa BBC Regina Mziwanda amezungumza nao: