Tazama: Mwanajeshi apiga Saksafoni hata baada ya kuanguka na kuzirai katika gwaride
Tazama: Mwanajeshi apiga Saksafoni hata baada ya kuanguka na kuzirai katika gwaride

Mwanachama wa bendi moja ya jeshi alikuwa mmoja wa askari kadhaa waliozimia wakati wa mazoezi ya kuelekea Trooping the Colour wikendi ijayo.
Alipopata fahamu zake na kusimama aliendelea kucheza kifaa hicho kabla ya wenzake kufika eneo hilo na kumuondoa
Tukio hilo lilitokea wakati ambapo kuna joto kali mjini London.
Mwanamfalme William baadaye alitweet: "Shukrani kubwa kwa kila askari ambaye alishiriki katika zoezi la majaribio la Mapitio ya Kanali asubuhi ya leo kwenye joto. Hali ngumu lakini nyote mlifanya kazi nzuri sana. Asante. W."



