TFF: Tanzania bado ina nafasi ya kufanya vizuri
TFF: Tanzania bado ina nafasi ya kufanya vizuri
Kufuatiwa kusimamishwa kwa Kocha mkuu wa Tanzania Adel Amrouche hapo jana kutokana na maamuzi ya shirikisho la mpira barani CAF, Msemaji wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa bado Tanzania ina nafasi ya kufanya vizuri kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Zambia.
Tanzania imecheza mechi moja dhidi ya Morocco na kucharazwa kwa goli tatu.
Adhabu ya kocha wa Tanzania ilitolewa baada ya maafisa kutoka Shirikisho la Soka la Kifalme la Morocco (RMFF) kuwasiliana na Caf kulalamikia matamshi yaliyotolewa na Amrouche.



