Ndani ya kambi za IS nchini Syria: 'Sikujiunga na IS. Nilikuwa na miaka 10 tu'

Maelezo ya video, Ndani ya kambi za Syria: 'Sikujiunga na IS. Nilikuwa na miaka 10 tu’
Ndani ya kambi za IS nchini Syria: 'Sikujiunga na IS. Nilikuwa na miaka 10 tu'

Kufuatia kushindwa kwa kundi la Islamic State (IS) mwaka wa 2019, maelfu ya watu, wakiwemo wanawake na watoto walizuiliwa wakati eneo linaloshikiliwa na IS nchini Syria lilipokombolewa.

Wengi ni raia wa kigeni. Mmoja wao ni "Asim", 19, kutoka Tunisia, ambaye alikuwa na umri wa miaka 10 tu aliposafiri kwenda Syria na kaka yake, ambaye alijiunga na IS.

Mwandishi wa BBC Kiajemi Nafiseh Kohnavard alipewa fursa adimu ya kutembelea kambi na vituo vya kizuzia watu kaskazini mwa Syria.