Macron na Tshisekedi wabishana hadharani juu ya Rwanda
Macron na Tshisekedi wabishana hadharani juu ya Rwanda
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amemaliza ziara yake ya siku mbili huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo alijadili hali ya usalama na mwenyeji wake Rais Félix Tshisekedi, ambaye ameitaka Ufaransa iilaani Rwanda moja kwa moja kwa tuhumu za kuwaunga mkono waasi wa M23, jambo ambalo Macro hakufanya.
Macron alimwaambia Tshisekedi kwamba jukumu la kuimarisha usalama mashariki mwa Kongo ni la serikali ya Kongo kwanza kabla ya kunyoosha kidole kwa nchini nyingine.