Watu wa Jinsi Mbili:‘Watoto wa jinsi yangu wanaanza kubaguliwa baada tu ya kuzaliwa'

Maelezo ya video, Watu wa Jinsi Mbili:‘’Baba yangu alitoroka nilipozaliwa, sijawahi kumuona na sidhani kama

Hakuna kitu kinachokatisha tamaa kama mtu kuteseka kwa jambo ambalo liko nje ya uwezo wake. Nazungumzia jamii ambayo imekuwa nadra sana kuzungumziwa hasa kwa Afrika Mashariki.

Watu wa jinsi mbili, ni watu wa kawaida kama wale wengine ila madhila wanayopitia ni ya kuvunja moyo hata ingawa hali yao inahusisha maumbile ya Rabana.

Mwandishi wa BBC Asha Juma alizungumza na watu wawili waliozaliwa na jinsi mbili akiwemo Daktari Denis Wamalwa, mtu wa kwanza wa jinsi mbili kushikilia ofisi ya serikali nchini Kenya na mwathirika ambaye kwa leo tumempa jina la Samuel kwa sababu ya usalama wake ili kutathmini kile wanachopitia.