Ed Sheeran aonya wasanii kulimbikiziwa madai yasio na msingi ya hakimiliki

Maelezo ya sauti, Ed Sheeran aonya wasanii kulimbikiziwa madai yasio na msingi ya hatimiliki

Ed Sheeran ameonya kuwa wasanii wa pop hawapaswi kukubali kutumiwa kuwa "walengwa rahisi" kwa madai ya haki miliki baada ya kushinda kesi yake mahakamani na waandishi wa wimbo ambao walidai kuwa aliiba maneno yao.

Jaji wa Mahakama Kuu aliamua mwimbaji huyo hakuwa amenakili sehemu ya wimbo wake, Shape of You, kutoka Oh Why, wa Sami Chokri.