Tuzo ya Nobel: Joto la jua au kukumbatiwa ni tiba ya maumivu
Kumbe kuna umuhimu wa binadamu kukumbatiana kuboresha afya yetu. Sasa Wanasayansi ambao waligundua jinsi miili yetu inahisi joto la jua au kukumbatiwa kwa mpendwa wameshinda Tuzo ya Nobel.
David Julius na Ardem Patapoutian, kutoka Marekani wanasema Matokeo yao yanaweza kusababisha njia mpya za kutibu maumivu. Hivi wewe huhisi vipi ukikumbatiwa? Sema nasi kwenye BBC facebook Swahili