Seven: Si kawaida kwa mwanamke kufanya kazi hizi na si tatizo la Afrika pekee
Christine Mosha au maarufu kama Seven ni Mtanzania ambaye ameteuliwa na Kampuni ya Sony Music Entertainment Africa, kuongoza kitengo cha Masoko na Maendeleo ya Wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Aidha Seven ni miongoni mwa wanawake wachache barani Afrika ambao wanafanya kazi ya kusimamia vipaji hususani muziki.
Katika miaka 16 ya kufanya shughuli hii anasema si rahisi hasa ukiwa mwanamke.