Christine Shusho:'Hakuna maisha bila shida lazima kuvumilia'
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha McGrill mwaka 2015 ulionesha kwamba viwango vya talaka katika mataifa mengi chini ya jangwa la sahara kupunguka au kusalia ilivyo.
Japo mojawapo ya sababu ambazo utafiti huu ulitoa ni kuwa ndoa nyingi na talaka katika mataifa haya haziyajarekodiwa.
Hata hivyo ndoa na talaka ni mambo ya kawaida katika maisha na pia ni mambo ambayo huchukuliwa kwa uzito mkubwa.
Msanii wa nyimbo za Injili Christina Shusho amezungumza na mwandishi wa BBC, Scolar Kisanga katika makala ya Amka na BBC na kufafanua maneno aliyoyasema hivi karibuni kwamba yeye haamini katika talaka na pia wanandoa wanapaswa kuvumiliana.